Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa Safari zitazoanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi,majaribia hayo yameongozwa asubuhi ya leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba dirisha la pili kutoka kulia,akiangalia nje wakati wa majaribio ya mabehewa sita kati ya kumi na mbili yatakayofanya safari zake kutoka Station mpaka Ubungo kuanzia mwezi wa Kumi mwaka huu,Treni hizo zitasaidia wananchi katika usafiri jijini Dar es Salaam.
Naibu Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba anayeongea na simu ,akiwa ndani ya behewa mojawapo kati ya mabehewa sita yalifanyiwa majaribio leo asubuhi,treni hiyo itakuwa ikifanya safari za safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo na inatarjiwa kuanza mapema mwezi wa Kumi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba,akipanda treni wakati wa majaribio ya Mabehewa sita ya treni kati ya mabehewa kumi na mbili yanatogemewa kutumika na Shirika la reli Tanzania(TRL). Treni hizo zitakayofanya safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo,mapema mwezi wa Kumi.
Baadhi ya wananchi wakipanda katika behewa moja kati ya Sita yaliyofanyiwa majaribio mapema leo kutokea Station mapaka Ubungo (km 12).
No comments:
Post a Comment