Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa TBL,Steve Kilindo(kulia) akimkabidhi mfano wa
hundi ya thamani ya shilingi milioni 51.6 mkurugenzi wa kampuni ya Dr
Gogo Engeneering, Godwin Kallaghe (mwenye kofia) kwa ajili ya shughuli
ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa futi 120 katika Kata ya Makanya,
wilayani Same, Kilimanjaro hivi karibuni. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David.
Wananchi
katika Kata ya Makanya, wilayani Same wakishuhudia zoezi la utolewaji
wa hundi ya kiasi cha sh. milioni 51.6 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima
cha maji.Hundi hiyo imetolewa na kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
Wananchi
pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa TBL, wakiomba dua katika eneo
ambalo kisima chenye urefu wa futi 120 kinachimbwa marabaada ya TBL
kutoa kiasi cha sh. mil. 51.6 kwa ajili ya shughuli za uchimbaji huo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dk.
Mathayo David akizungumza na wananchi katika eneo la Makanya ambako
kisima chenye urefu wa futi 120 kinachochimbwa kwa msaada wa sh. mil.
51.6 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili a shughuli hiyo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Dr. Gogo Engeneering Company Ltd,Godwin Kallaghe
akizungumza na wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa mfano
wa hundi,Kallaghe amesema kazi ya uchimbaji wakisima hicho utafanyika
kwa muda wa wiki tatu hadi kukamilika kwake.

No comments:
Post a Comment