Meneja wa Tanesco Mkoa wa Temeke
Richard Mallamia, akionyesha namna umeme ulivyounganishwa kimakosa na
wezi huko Toangoma.
| Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kigamboni Mhandisi Eusterd Edward akimuonyesha namba za nguzo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Temeke Mhandisi Richard Mallamia (kulia) na Mhandisi wa Mkoa huo Ebenezer Fue. |
Hapa gari la Tanesco liking'oa nguzo
hizo za wizi.
Fundi akiondoa mita ya wizi kwenye
nyumba hiyo iliyokutwa imeunganishwa umeme kinyemela.
Baadhi ya nyaya zilizokutwa na jeshi la
polisi kwenye moja ya nyumba zilizokuwa zikiunganishiwa umeme kinyemela.
Wahandisi wa shirika hilo wakiangalia
baadhi ya nguzo zilizo katwa na wezi hao.
Na Said Powa
KATIKA
haliisiyokuwa yakawaidaShirika la umemeTanzania (Tanesco) MkoawaTemeke jijini
Dar es Salaam limegundua wizi wa ainayake baada ya kukamata nguzo zaidi ya 6
nanyayazake zaidi ya mita 600 zilizo sambaziwa umeme mitaani
na wezi kwa kushirikiana na wenye nyumba.
Akizungumzia
tukio hilo mbele ya waandishi wahabari wakati wa operesheni hiyo iliyofanywa kwenye
eneo la Toangoma Kigamboni jijijini humo Meneja wa Mkoa wa Tanesco Temeke Mhandisi
Richard Mallamia, alisema wamepenyezewa taarifa za wizi huo na raia wema natayari
kabla ya kufika kwenye operesheni hiyo uchunguzi wa awali unaonyesha kuna uwezekano
wa watendaji wa shirika kuhusika na tukio hilo.
Aidha
kwenye zoezi hilo ambalo lilikuwa kama la kushitukiza kwenye eneo la Toangoma
Masaki mmiliki wanyumba moja ambayo walikutwa mafundiwakiendelea na ujenzi aliunganisha
umeme kwakushirikiana na wezi hao kwa kujichomekea nguzo zake mbili hadi kufikia
nyumbayake ikiwa niumbali wa zaidiyamita 200 bila ya kufuata taratibu za shirika.
Akielezea
tukio hilo Mhandisi wa Mkoa huo Ebenezer
Fue, alisema pamoja na kutofutwa kwa taratibu za uunganishaji kwenyeshirika
lakinipia uunganishwaji wenyewe wa umeme ni wahatari kwakua haujazingatia viwango
vya kitaalamu vinavyokubalika.
“Hizi
nguzo zilizotumika hapa sizo za kusambaza umeme hukumtaani ndiomaana unaona wamezikatakata
ili waweze kuzituumia na hatabaadhi ya viunganishi vya kwenye nguzo haviunganishwi
kama hivi inavyoonekana,” alisema Fue.
“Hivi
vifaa vyote ni vya shirika lakini vimefikaje huku nanani kavileta huku, ndio hatua
hii tuliyoanza kuchukua sasa itatubainishia, ingawa tumeanza kutajiwa majina ya
baadhi ya wahusika wa kazi hii ambao wamo ndani ya shirika lakini nimapema sana
kuwataja kwasasa ngoja tuendelee na kukusanya taarifa zaidi” Mhandisi Malamia
alifafanua.
Kwa
mfumo huohuo operesheni hiyo ilibaini maeneomengine mawili kwenyekitongoji hicho
cha Toangoma ambako nako pia zimechomekwa nguzo nne zikiwa na nyayazake hukuwateja
hao wakisubiri hatua za mwisho kuingiziwa umeme ndani ya nyumbazao huku shirika
hilo likiwa halina hata taarifa za wateja hao.
Lakini
jambo baya zaidi na la kusikitisha linalofanywa na wezi hao wamekuwa wakikata nyaya
kwa wateja waliounganishiwa umeme kihalali kwenye mitaa na kuchukua nyaya zake kwenda
kuunganishia watu wengine huku wakiwakosesha umeme watu wengine.
Msafara wa shirika hilo uliongozwa na Meneja wa Wilaya ya Kigamboni Injinia Eustard Edward,ulifika hadi eneo ambalo familia kadhaa zimekosa umeme baada ya nyaya zake kuibwa na kwenda kuunganishiwa watu wengine.
Kwamujibu
wataratibu za shirika hilo ‘service line’ za umeme zote zinakuwa tayari kwenye ramani
ya shirika kwenye eneo lote la kusambaza umeme lakini wateja walikutwa na umeme
huo hata kwenye shirika ramani hiyo haipo kwa hiyo mojakwamoja haoni wezi na
wanpaswa kuchukuliwa hatuaza kisheria.
Hatahivyo
Mhandisi Mallamia alisema wizi huo umelitia hasara shirika kwasababu hatanguzo zilizotumika
kusambaza umemehuo sio nguzo za umemewa mtaaani ni nguzo kubwa za kusambaza umeme
kwenye laini kubwa, na ndiomaana wamelazimika kuzikata zaidi ya maramoja ili ziweze
kuendana sawa ambapo alisema kufanya hivyo nihasara kubwa kwani nguzo moja
pekee thamani yake karibu Tsh 2 Millioni.
Aidha
Mallamia amewapongeza watanzania wenye uchungu na shirikalao kwakutoa taarifa za
wizi huo na kuwataka kufanya hivyo mara kwa mara ili kufichua uovu huo.
Tangu
Shirika hilo kufungua ofisi za kanda Mikoa na Wilaya na kuwa na Mameneja wenye
meno kumekua na ufanisi kiutendaji ndani ya shirika kwa kuweza kufuatilia
matukio kwa haraka.
Hizi ni habari za uwongo Huyu bwana Fue pia ni mmoja ya watu wanao kuala mali ya uma hapa Temeke nasema kuna miundo mbinu kibao inayo washibisha kinyemela na kwafaida kubwa kwao wnauza vitu vingi kwa faida yao binafsi wanaungnisha kwa manufa yao binafsi hawa wanao watolea tarifa niwale walio unganishiwa na watu wengine ambao hawakuwapa chochote ninaushahidi wa wazi kabisa kuna malipo mengi ya mamilioni hupokea kwamakampuni fulani kinyemela bila usajili halali wa kampuni niko tayari kusirikiana na yule atakae kua tayari kuni tafuta kwenye email yangu gmjemas@yahoo.com nimengi yanayo fanyika Tanesco ubungu nawao ndio kweli wamegeuza shirika hilo shamba la bibi naimekua ni mali yao wanalitia shirika hasara kwa makusudi bila kujali kwa visingizio kibao mkoa wa temeke unaongoza kwa ushagidi mwingi naipenda tanzania nawapenda ndugu zangu watanzania nilazima tujikwamue katika utumwa huu wa wahuni hawa alio geuza shirika hili kua mali yao wakifanya wanavyo taka.
ReplyDeleteHuwezi kuamini kwa wewe usie jua utakubali habari za watu hawa eti mwandisi et meneja wakanda hawa ni wahuni wanawaibia watu vibaya hawna utu kabisa wala hawana mapenzi kwa shirika nakuambia kwa ushahidi binafsi nilisha fichua mengi ndani ya shirika hilo watu wakasimamishwa kazi na baadae wakarejeshwa kazini na kulipwa pesa nyingi tuu ushahidi upo leo utawasifia kwa lipi wana wadaganya sana viongozi maana hawahui lakini mimi nimesha umwa nyoka kwenye shirika hili la uma na sasa bado nahitaji niwajibike tena hadi mwisho niukweli usio pinmgika kuna pesa kibao zinalipwa kwa watu binafsi haziingii kwenye shirika mimi kwa sasa sina kazi nyingine nitafanya kila niwezalo hadi nilikomboe shirika hili kutoka mikononi kwa wajukuu wa bibibi ambao wanalitafuna wanavuna bila kupanda haiwezekani wezi hawa lazima watokomezwe matukio ni mengi hata lile la kiwanda cha wachina kule mbagala mimi nilisha liripoti siku nyingi nikawapeleka na watendaji lakini walijijengea mtandao wakaendelea kula pesa kunakiwanda kingine chan'ombe nilisha kiripoti nawtu wakasimamishwa kazi lakini hakuna kilicho badilika wanatumia kama kawaida na watu wanavuta pesa hakuna ubishi kwa mba wakubwa hawa wanajua kwanini nasema hivi unapo toa tarifa kamahii kwa meneja au unapo taka kuzungumza nae kwania ya kumpa muelekeo haonyeshi ushirikiano kwanini usikubali kua yeye ni mmoja wao mtuu utakuaje kiongozi wa shirika la uma usitake kuwasikiliza wananchi unainua mabega tuu nakujivuna Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika tumenyonywa kiasi chakutosha sasa tunataka mabadiliko ya kweli naitwa Gregory Emmanuel Mjema Niko Dar es salaam
ReplyDelete