Mkurugenzi wa Kampuni ya Edge Entertainment ambao ni waandaaji wa Tamasha la Muziki Tanzania,Edwin
Ngere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
wakati wa kutangaza siku ya Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa siku
mbili kuanzia kesho Septemba 28 na 29 katika viwanja vya Leaders
Club,jijini Dar.Wengine pichani ni Baadhi ya wanamuziki wa Bendi mbali
mbali ambazo zitashiriki Tamasha hilo pamoja na Balozi wa Tamasha
hilo,Jacqueline Wolper (pili kulia).
Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya Wazee Sugu,King Kikii (pili kushoto) akiongea
kwa msisitizo juu ya jinsi alivyojiandaa yeye na bendi yake kuonyesha
umahiri katika Tamasha hilo la Muziki wa Dansi hapa nchini.Tamasha hilo
litafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho Septemba 28 na 29 katika
viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo wa kutambulisha siku ya Tamasha la Muziki wa Dansi hapa nchini.





No comments:
Post a Comment