Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Redd's
Miss Tanzania,Hashim Lundenga (pili Kushoto) akizungumza na Waandishi wa
Habari kwa Msisitizo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo
wakati wa kutangaza kuanza kwa kambi rasmi ya Redd's Miss Tanzania 2012
na ukumbi utakaofanyiwa Shindano hilo mwaka huu ambao ni Blue Peal
uliopo ndani ya Jengo la Ubungo Plaza,jijini Dar es Salaam.Wengine
Pichani toka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria
Kimaro na kulia ni Miss Tanzania 2011,Salha Israel.
Meneja wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro akiongea mbele ya
waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga wakiwa kama
wadhamini wakuu wa Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania 2012.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akifafanua jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo,jijini Dar.
Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).
Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao. 2013.





No comments:
Post a Comment