Rais
na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mjane na
ndugu wa Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa
marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012
kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU. 

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.


No comments:
Post a Comment