Saturday, September 8, 2012

Noela Michael anyakua taji la Redd's Miss Ilala 2012

Redds Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena Munisi (kulia) na mshindi wa tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redds Miss Ilala 2012.

Noela Michael mwenye umri wa miaka 19, kutoka Tabata usiku wa kuamkia leoalitwaa taji la Redds Miss Ilala 2012 katika ukumbi wa Nyumbani Lounge,Namanga, Dar es Salaam.
Noela ambaye amemaliza kidato cha sita, anajiandaa kuingia Chuo Kikuu chaDar es Salaam (UDSM), aling’ara katika usiku huo ambao alipata upinzani mkalikutoka kwa Magdalena Roy Munisi mwenye umri wa miaka 21, ambae ni redds MissDar City Centre aliyeshika nafasi ya pili.
Kimwana Mary Chizi alikuwa ana usiku mzuri pia jana, kwani pamoja na kutwaataji la mrembo mwenye kipaji zaidi na kupata Sh. 500,000, pia alishika nafasiya tatu na kuungana na wenzake hao wawili kwenda Redds Miss Tanzania.
Katika shindano hilo liliosindikizwana burudani ya wasanii Wane Star, Chegge, T Africa kutoka Temeke, Spencer Groupna Machozi Band, mshindi wa nne alikuwa Mecktilda Martin mwenye umri wa miaka19, kutoka Redds Dar City Centre na wa tano alikuwa mrembo Elizabeth Prettymwenye umri wa miaka 21 kutoka Ukonga.
Washiriki wengine ni Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris, WilminaMvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe na Phillios Lemi.

Kwa ushindi huo, Noela anayerithi taji la Salha Israel ambaye pia ni MissTanzania 2011, alijipatia kitita cha Sh. Milioni 1.5, wakati Magalenda alipataMilioni 1.2 na Merry 700,000.

Mecktilda na Elizabeth kila mmoja atapata 400,000 wakati wengine wote,Washiriki wengine ni Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris, WilminaMvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe na Phillios Lemikila mmoja atapata Sh. 200,000. Zawadi zote zinatarajiwa kutolewa katika ukumbiwa Nyumbani Lounge, sambamba na pati maalum.

Noela sasa anakabiliwa na changamoto situ ya kutetea tu taji la Redds Miss Ilala, bali kuendeleza rekodi nzuri yakanda hiyo katika Redds Miss Tanzania iliyowekwa na akina Hoyce Temu,Jacqueline Ntuyabaliwe, Angela Damas Mutalimwa na Salha.

Awali akizungumza ndani ya ukumbi huomratibu wa Redds Miss Kanda ya Ilala Gadna Habash alisema warembo wotewalioshiriki mwaka huu kupitia kanda ya ilala wameweza klupata fursa kubwa yakujifunza mambo mbalimbali yatakayowapatia mwanga katika maisha yoa hasa katikatasnia ya urembo nchini.

No comments:

Post a Comment