Thursday, September 6, 2012

Naibu Waziri Mkuu wa China afanya ziara TAZARA jijini Dar leo

 Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyenyoosha mikono)akiteta jambo na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa TAZARA wakati wakimsubiri Naibu Waziri Mkuu wa China, Mhe. Hui Liangyu aliyekuwa na ziara ya saa moja katika taasisi ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo na Kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi,Bw. John Mngodo.
Waziri wa Uchukuzi akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu katika Station ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Naibu Waziri Mkuu wa China alikuwa na Ziara ya kuangalia Namna Station hiyo inavyofanya kazi. Serikali ya China imetuma wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti wa namna ya kuboresha Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu(Mwenye Tai ya Bluu),akisalimia na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasilini kwenye stesheni hiyo.
 Bw. Miao Zhong mmoja wa watafiti waliotoka China akimuonyesha Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu(kulia kwa aliyejishika jicho) njia ya reli ilipoanzia kwa upande wa Tanzania. Naibu Waziri Mkuu wa China alikuwa na ziara katika Mamlaka hiyo leo asubuhi.
 Waziri wa Uchukuzi akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari(hawapo pichani),kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo na Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wa Wizara ya Uchukuzi,Bw.John Mngodo.
Naibu Waziri Mkuu wa China Mhe. Hui Liangyu(wa saba kutoka kushoto),akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Uchukuzi, baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasili katika station hiyo leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment