HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 18, 2012

FARU WEUSI WAONEKANA ARUSHA NA MWANZA

Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia cha (TBL) kanda ya kaskazini na wadau wa bia jijini Arusha wakigonganisha chupa wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa bia mpya ya FARU jijini Arusha,hivi karibuni.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia cha (TBL) kanda ya kaskazini wakifurahia uzinduzi wa bia hiyo mpya aina ya FARU.
Meneja Masoko wa TBL,Bi. Natalia Celeni (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Meneja Mauzo wa TBL wa kanda ya kaskazini,Kasiro Msangi (kulia) mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Kampuni hiyo kinachojulikana kwa jina la FARU .Uzinduzi huo umefanyika jijini Arusha hivi karibuni.
Meneja Masoko wa TBL,Bi. Natalia Celeni (kulia) akiyarudi magoma sambamba na Meneja Mauzo wa TBL wa kanda ya kaskazini,Kasiro Msangi wakati wa kusherehekea uzinduzi wa Bia Mpya ya FARU.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia cha (TBL) kanda ya kaskazini na wadau wa jijini Arusha wakiyarudi magoma kwa pamoja.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa mara nyingine tena imetingisha soko la bia hapa nchini kwa kuzindua bia ya aina yake na yenye hadhi ya kimataifa.

Bia hiyo iliyobeba jina la mnyama adimu, mwenye kila aina na sababu za kusifiwa “FARU” imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na utofauti wa kipekee katika muonekano na ladha.

Akizungumzia uzinduzi wa Bia hiyo ambayo kwa kuanzia imezinduliwa katika kanda za Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi Meneja wa bia hiyo,Bi. Kabula Nshimo alisema “Bia hii mpya inajulikana kama FARU DARK LAGER”, ni bia inayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu, inayoifanya bia hii kuwa laini na rahisi kunywa, bia ya Faru ina kilevi cha asilimia 5.2, Baada ya uzinduzi katika kanda hizo mbili, Faru itasambazwa nchi nzima. Tunaamini kuwa bia hii italeta mapinduzi makubwa katika soko la vileo hapa nchini. Alisema Kabula

Bia ya Faru Dark Lager inauzwa kwa shilingi 1,800/- tu kwa chupa, hivyo kuwapa fursa wadau na wapenzi wa bia kuipata kwa urahisi. Tumeipa bia hii jina adhimu la mnyama Faru ili kumuenzi mnyama huyo adimu mwenye nguvu, mvuto na thamani ya kipekee. Tuna imani kubwa kuwa wapenzi wa bia wataifurahia sana Faru Dark Lager. Aliongeza Bi. Kabula

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad