HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 7, 2012

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE MJINI DODOMA

Maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika Banda la Wizara hiyo katika Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma tayari kutyoa huduma kwa wageni watakaotembelea banda hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara Bw Ismael Mfinanga na Mkaguzi wa ndani wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Asia Mohamedi, wakipata maelezo ya kazi mbali mbali zinazofanywa na wajasiriamali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Gregory Teu (Kushoto), akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) waliopo katika maonesho ya 88 mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Vicent Kone akipokelewa na maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara alipotembelea banda la Wizara hiyo katika Viuwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Vicent Kone akipata maelezo ya bidhaa mbali mbali za mjasiriamali anayewezeshwa na na Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonesho ya 88 mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajasiriamali kutoka Mikoa mbali mbali nchini wakishiriki mafunzo yanayotolewa na taasisi mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Viwanmda na Biashara ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa tija. Mafunzo hayo hutolewa bure kila siku asubuhi kabla ya kuanza kwa maonesho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad