HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 9, 2012

Simba Day ilivyoadhimishwa leo uwanja wa Taifa jijini dar

Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya mabeki wa timu ya Nairobi City Stars ya nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kuadhimisha Tamasha la siku ya Simba (Simba Day) lililofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo liliandaliwa na klabu ya Simba na huwa linafanyika kila mwaka Agosti 8 kama ya leo na kushirikisha timu marafiki wa klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo timu ya Simba imefungwa magoli 3-1.
Mchezaji wa mpya wa Timu ya Simba,Mrisho Ngassa akijiandaa kupiga mpira mbele ya Mabeki wa timu ya Nairobi City Stars katika mchezo uliochezwa leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Simba (Simba Day) ambayo huwa yanafanyika kila Mwaka siku kama ya leo.Simba imefungwa Bao 3-1.
Danny Mrwanda wa Simba akijiandaa kumtoka beki wa timu ya Nairobi City Satrs.
Wachezaji wa Simba wakiwa hawaamini kitu kilichotokea uwanjani hapo.
Wachezaji wa Nairobi City Stars wakishangilia ushindi wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad