Katibu wa Taasisi na Jumuiya za
Kiisilamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu zoezi la Sensa linalotarajiwa
kufanyika Augost 26 mwaka huu, ambapo alisema waisilamu kamwe
hawatashiriki zoezi hilo na watakaa itikafu misikitini usiku wa Augost
25 na kusoma dua mpaka asubuhi.
Masheikh zaidi ya 40 ktoka kwenye
taasisi na jumuiya na mabaraza ya kiisilamu nchini ambao pia ni maimamu
wa misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam wakiwa wakimuunga mkono
Katibu wa taasisi na Jumuiya za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda wakati akitangaza maelekezo kwa waisilamu juu ya namna ya kuwajibu
makalani wa sensa.
No comments:
Post a Comment