Tuesday, August 21, 2012

SAKATA LA GAZETI LA MWANAHALISI LACHUKUA SURA MPYA.

Mwnyekiti wa MISA TAN Mohamed Tibanyendera, akizungumza na waandsihi wa habari kuhusu hatua wanazozichukua dhidi ya Serikali kutokana na kulifungia gazeti la Mwanahalisi.
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya asasi za kiraia inayoshughulikia harakati za kulifungulia gazeti la MwanahalisiMarcossy Albanie akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini kuhakikisha wanapata kila tukio.

KAMATI ndogo iliyoundwa na taasisi nne za kiraia nchini ambayo inaratibu mchakati wa kupigania haki ya kufunguliwa kwa gazeti la Mwanahalisi leo imeipa serikali siku saba kuliruhusu gazeti hilo kuendelea kuchapishwa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Marcossy Albanie, amesema hawana sababu yakwenda mahakamani juu ya jambo hilo kwasababu hata serikali haikutumia njia hiyo ya mahakamani kwani ilikuwepo badalayake wametumia sheria kandamizi ya vyombo vya habari inayopigiwa kelele na wadau wa habari.
Kamati hiyo inayoungwa mkono na taasisi tano za kiraia baadhi ya taasisi hizo ni MISA TANZANIA, TANZANIA HUMANRIGHTS DEFENDERS COALITIONS NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) imeitaka serikalikutekeleza madai yafuatayo.
1.Kuitaka serikali kulifungulia gazeti la Mwanahalisi maramoja.
2.Serikali badala ya kushughulikia Watetezi wa haki na wanahabari wanaofichua uovu ishughulike na wahalifu waluiomteka Dk.Ulimboka.
3. Serikali iache kabisa na ukandamizaji huu wa haki na uhuru wa habari.
WAANDISHI WA HABARI WAOMBWA YAFUATAYO SERIKALI ISIPO TEKELEZA HAYO:
Kutochapisha habari yeyote itakayo wahusu Waziri wa habari wa Wizara hiyo na Naibu wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
Kusimama kidete kuunga mkono harakati hizo hadi zinapata ufumbuzi wake.
Ikumbukwe kesi Na.34/2009 iliyofunguliwa tangu 2008 kupinga sheria ya magazeti ya 1976 iliyotumika kufungia Mwana Halisi haijasikilizwa mpaka sasa.
Mwisho:

No comments:

Post a Comment