Monday, August 13, 2012

MICHUANO YA MBIO ZA BOTI YA ‘MERCEDES CUP 2012′ YARINDIMA JIJINI DAR

Washiriki wa mashindano ya Mercedes Cup 2012 ya Boti zinazokwenda na Upepo (Sailing Boat) wakiwa wamekusanyika Yatch Club jijini Dar kabla ya kuanza mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors yanayofanyika kila mwaka.
Boti zinazotumika katika mashindano hayo.
Washiriki wakianza mashindano hayo kuzunguka fukwe karibu na kisiwa cha Bongoyo.
Boti iliyombeba Refarii wa mashindano hayo pamoja na wasimamizi wengine.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed(katikati) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) pamoja Catamaran Representative wa Dar es Salaam Yatch Club Andrew Boyd.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimkabidhi zawadi Refarii wa mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akikabidhi zawadi kwa moja ya timu iliyoshiriki mashindano hayo na kushika nafasi ya nne.
Washindi wa tatu David na Sarah Scott wakipokea zawadi na tuzo.
 Washindi wa pili Paul na Kim Troll wakipokea zawadi kutoka CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akikabidhi Kombe kwa timu ya washindi wa kwanza wa mashindano ya Boti zinazokwenda kwa kutumia upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 Al Bush na Jeppe yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh. Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (Kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) katika picha ya pamoja ya washindi wa kwanza hadi wa tatu walioshiriki mashindano ya Boti zinazokwenda kwa upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 baada ya kukabidhiwa vikombe na zawadi zao yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.

No comments:

Post a Comment