HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 3, 2012

Mh. Lowassa akabidhi jozi za kanzu na mifuko ya tende kwa waislamu wa Monduli leo

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi sehemu ya tende kwa Masheikh wa Mji wa Monduli kwa ajili ya Ftar katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.kutoka kushoto ni Sheikh wa Mto wa Mbu,Sheikh Nasib Idd Nasib Mnyema,Katibu wa Bakwata wilaya ya Monduli,Idd Idoya,Ustadh Swalehe Ramadhan na sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba.Makabidhiano haya yamefanyika leo asubuhi nyumbani kwa Mh. Lowassa,Monduli.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipena mikono na Mashekh wa Wilaya ya Monduli baada ya makabidhiano ya katoni kadhaa za tende pamoja na jozi 100 za kanzu kwa ajili ya Waislam wa Monduli.Akipokea msaada huo, Sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba, alimshukuru mh Lowassa kwa utaratibu wake huo ambao amekuwa akiufanya kila mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislam wa Monduli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad