Monday, August 6, 2012

Kilio cha Mdau kuhusiana na utaratibu Mbovu wa Basi la Sumry

Mambo vipi Mzee wa Mtaa kwa Mtaa,

Mie ni Mdau mzuri sana wa libeneke lako la Mtaa kwa Mtaa,kwani umekuwa ukitupatia vitu adimu ambavyo havipatikani katika libeneke lolote hapa nyumbani,Hongera sana kwa kweli.

Leo nami nimekuja na langu la kuhusiana na usafiri wa mabasi yaendayo mikoani ya kampuni ya Sumry, hasa haya yanayopiga ruti ya Dar - Bukoba.

Nikiwa ni mmoja wa abiria tunaosafiri na moja ya mabasi hayo kutokea Dar kwenda Bukoba siku ya leo  ambapo tumetoka Dar saa 6 mchana badala ya saa 12 asubuhi kama inavyokuwa kawaida,huku tupakiwa kwenye gari iliyofika leo hii hii kutokea huko huko Bukoba,(sasa sijui hata hiyo service wameifanya saa ngapi kwenye gari hiyo na je Dereva kabadilishwa au ni yule yule?).

Halafu wahusika hawana customer care nzuri yani wametuacha tumekaa chini ya mti hakuna viti na wala hakuna anayekuja ku-appology.

Na hii sio leo tu na jana nasikia waliondoka saa 6 na ukweli ni kwamba leo sio mwisho pia kwa maana basi lililofika leo na kugeuza leo ilitakiwa ligeuze kesho asubuhi kwa hiyo abiria wa kesho itawalazimu pia kusubiri gari itakayofika kesho hiyo hiyo.

Na inaonekana kuwa hali hii imezoeleka kwa kuwa hata polisi wa ubungo na maafisa wa Sumatra walioko hapo hawakushangaa abiria tulipowapelekea malalamiko yetu kwao. Yaani Nimechukizwa sana ukizingatia kuwa hii ni kampuni kubwa lakini inaweka rehani roho za watu kwa kutopumzisha gari na huenda hata dereva hapumziki.

Kwa leo ni hayo tu.
Mdau wa Mtaa kwa Mtaa Safarini,Bukoba.

Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

No comments:

Post a Comment