Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akitambulishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kwa viongozi wa TRL na wale wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli TRAWU mara alipowasili katika Karakana ya TRL.
Waziri Mwakyembe akipata maelezo ya jinsi ya ukarabati wa mabehewa 14 unavyoendelea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu wa kwanza kulia.
Baadhi ya mabehewa yanayokarabatiwa kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa Wakazi wa jiji la Dar.
Viberenge viwili malum vikijitayarisha kuondoka kuelekea Ubungo wakati wa ukaguzi wa njia ya reli ambayo itatumiwa na treni ya abiria ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam inayotarajiwa kutoa huduma hapo Oktoba mwaka huu.
Faraja kubwa kusikia jambo hili mwishoe linatekelezwa. Nilihusika binafsi kutafiti kwa nini hili lisiwezekane, nimeongea na mkurugenzi wa Tazara aliyenipa mwanga mkubwa sana, na kwa miaka kadhaa hili jambo lilifubaa kwa sababau za rushwa, wawekezaji walikuwepo na kila kitu kipo lakini watu (watumishi wabaya wa sirikali) wakalikalia, yaani bila kuhakikishiwa asilimia 10 yao waligoma kupitisha hivyo kutuacha wananchi tukitaabika. Hongera kwa wadau wote husika waliowezesha hili kufanikiwa. nasubiri sana hili kwa hamu..Kwa upande wa ajali huu usafiri wa reli utatupunguzia ajali za kizembe zilopoteza maisha ya raia wasio na hatia. kwa upande wa uchumi hii ni hatua muhiu sana ya kwenda na wakati maana usafiri ni sehemu ya mawasiliano na kukiwa na usafiri wa uhakika na s,alama basi hata uchumi utasonga si kwa zile takwimu za ki-IMF bali hata wananchi wataona jinsi uchumi unavyotengemaa. Tuko pamoja, Mungu ibariki Tanganyika mungu Ibariki Afurika. Ashe
ReplyDelete