Precision Air, shirika la ndege linaloongoza Tanzania leo imezindua tovuti yaompya pamoja na kampeni maalum ya mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitterili kuweza kuimarisha uhusiano mzuri na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Akizungumza kwa njia yaYouTube jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Bi. Lilian Massaweamesema kwamba tovuti hiyo mpya imetengenezwa mahususi kwa ajili ya wateja ilikuweza kuwapatia urahisi wa kupata taarifa mbali mbali za kampuni, nakukamilisha mipango yao ya kusafiri kwa ufanisi.
“Kati ya vituvilivyoongezewa katika tovuti hii mpya ni taarifu muhimu kuhusu mtandao wetuwote wa sehemu 16 tunazosafiri, bila kusahau chombo maalumu ambayo mteja wetuanaweza kutumia kununulia tiketi yake ya safari akiwa sehemu yeyote dunianikupitia kadi za Visa na Master bila hata kufika ofisi za Precision Air kwa beinafuu zaidi maana hata katwa makato ya huduma (service fee),” alisema Massawe.
Tovuti hiyoinayopatikana pitia www.precisionairtz.com pia inakuja na fomu ya malalamiko ya wateja ambayo itaruhusu kampuni kupata taarifaza moja kwa moja kutoka kwa wateja wao kokote waliko.
Wakati huo huo, shirikahili la ndege limezindua kampeni maalumu ya mitandao ya kijamii kupitiaFacebook, Twitter na YouTube ili kuweza kwenda na soko la utandawazi wa kisasawa njia ya mawasiliano kupitia intaneti utakaoweza kuwaongezea uwepo mkubwazaidi kwa wateja wao.
“Kampeni yetu yamitandao ya kijamii inalenga kuongeza uaminifu na ushirikishwaji wa moja kwamoja kwa wateja wetu. Pia tunaamini kwamba kupitia mitandao hii ya Twitter,Facebook na YouTube, kutakuuza idadi ya wateja kuwa wengi zaidi watakaotembeleatovuti yetu, pamoja na kutupa fursa ya kuwafahamu wateja wetu kwa undani zaidi,”alisema Afisa Mawasiliano wa Precision Air, Amani Nkurlu.
“Tunapenda kuwaalika washabikiwetu wote kutembelea mtandao wetu wa Facebook kupitia www.facebook.com/PrecisionAirTz na kutufuata katika Twitter kupitia www.twitter.com/PrecisionAirTz ili kuwezakuwasiliana nasi na kujishindia zawadi mbali mbali kutoka kwa Precision Air,”Nkurlu aliongeza.
Mwaka 2011 Precision Airilizindua chombo maalum ya kukata tiketi kupitia mtandaoni yaani InternetBooking Engine yenye jina la Click and Fly kwa dhumuni la kurahisisha huduma yaukataji tiketi kwa msafiri kupitia kadi za Master na Visa. Mwaka 2010 shirikapia ilizindua PW-SMS, bidhaa ambayo inamuwezesha msafiri kufahamu kuhusumipango yake ya kusafiri kwa kupitia simu ya kiganjani tu.
Precision Air hivi sasainasafiri kwenda miji mikuu yote ya Tanzania ikiwemo Mwanza, Bukoba, Musoma,Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar, Mtwara na Dar es Salaam. Kikandainasafiri kuelekea Nairobi na Mombasa nchini Kenya, Entebbe nchini Uganda,Hahaya nchini Comoros, Lubumbashi nchini Congo DRC, Lusaka nchini Zambia naJohannesburg nchini Afrika Kusini.

Precision wapo juu. Laiti kama *TC wangekuwa creative namna hii wangelifanikiwa. Sio tu kwa upande wa marketing initiatives ila kwa upande wa equipment (ndege zinazopaa) na social responsibilities. Wateja wa sasa hivi wanapenda kuona makampuni wanayonunua kwao yanatilia kipaumbele ajira kwa wazalendo na jamii inayowazunguka. *TC jifunzeni
ReplyDelete