Sunday, July 29, 2012

Msama aendelea na zoezi la kukamata wezi wa kazi za wasanii

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari ‘cd’ feki zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 20 zilizokamatwa eneo Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

MKURUNGEZI wa Kampuni ya Udalali Msama, Alex Msama akishirikiana na Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata watu 8 baada ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya milioni 25.

Akizungumza Dar es Salaam jana Msama alisema wiki iliyopitawalianza zoezi la kukamata watu wanaozidurufu kazi za wasanii mbalimbali ambazo wanauza kwa faida yao.
Msama alisema wakiwa maeneo ya buguruni sheli, walifanikiwa kuzikamata kazi hizo zikiwa zinauzwa kwa bei ya chini.
Alisema kuna baadhi ya kazi hata mtaani hazijaanza kutoka lakini wao wanazo na wakiuza kwa shilingi 1000 kila moja.
"Tumekuta kazi mbalimbali kama vile za muziki wa Injili, Movies, nyimbo za bendi muziki wa ndansi na taarab" alisema Msama.
Alisema licha ya kukamata CD hizo za kusikiliza na kuonesha ilifanikiwa kukamata mashine moja ya kudurufu. Msama alisema katika zoezi hilo waliwakamata watu nane wakiwa wanauza kazi hizo.
Waliokamatwa ni Halfan Bakari, Hassan Bakari, Hemed Mohamed,Patrick Peter, Hashraf Rajab, Mkoya Peter na Khamis Athuman. Msama alisema watuhumiwa hao wote wapo katika kituo cha Polisi Buruguruni kwa ajili ya uchunguzi. 

Wakati huo huo Kampuni ya Msama Promotions, imekamata watu watatu wakiwatuhumu kuuza kazi za wasanii kinyume na taratibu.

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema vijana hao walikamatwa katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Waliokamatwa katika tuklio hilo ni Malik Sultan, Ally Msangi, Edward Michael na Sijali Andrew ambao walikuwa na CD feki 322 za wanamuziki mbalimbali na wasanii wengine. 

Msama alisema zoezi la kukamata wezi wa kazi za wasanii linaendelea kwa kufanya uchunguzi katika maeneo sugu ambako hatua inayofuata ni kwa wale wanauza kazi hizo mikononi.

Aidha Msama analishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa timu ya vijana wake wanaosaka wezi wa kazi za wasanii.

No comments:

Post a Comment