Saturday, July 21, 2012

kibanda cha kusimama abiria kituo cha Kinondoni Kanisani Jijini Dar kulikoni???

Katika pita pita zangu za kuhakikisha libeneke la Mtaa kwa Mtaa halitoki kapa,niliibuka mitaa hii ya Kinondoni Kanisani,jijini Dar mchana wa leo na kukuta Kibanda cha Kupumzikia abiria wakati wakisubiria usafiri wa daladala kikiwa kimepiga mueleka huku watu wengine wakiwa wamekaa juu ya kibanda hicho.Nilipojaribu kuuliza kwa jamaa waliopo jirani na kituo hicho waliniambia kuwa Kibanda hicho kina zaidi ya miezi mitatu tangu Kipige mweleka na hakuna mtu hata mmoja anaetaka kukishughulikia na haifahamiki ni kwanini wamekichunia namna hiyo.

No comments:

Post a Comment