Sijui kuna kamchezo gani kanakoendelea hapa jijini Dar,maana uhifadhi taka wa namna hii umekuwa ukiendelea siku hadi siku katika maeneo mbali mbali ya jiji na sioni hatua zozote zikichukuliwa na wahusika.sifahamu wanachokiwaza,kwani haiwezekani waendelee kukaa maofisini mwao huku mifuko ikiendelea kutuna na ili hali kazi iliyowafanya wakae huko hawaifanyi.
hebu oneni jamani,kweli ni hali hii??
eehhh.... cheki na hapa,hii ni kona ya Mwananyamala.
haya huku pia.na hizi ni baadhi tu ya picha za maeneo hayo.naendelea na kupitia na maeneo mengine na mapicha kibao nitayaweka hapa.





No comments:
Post a Comment