Libeneke la Mtaa kwa Mtaa leo liliibukia maeneo ya Mburahati jijini Dar na kukutana na hii ya Mama huyu akimfundisha mwanae kuendesha Baiskeli katika uwanja wa Mburahati kwa Jongo,ili aweze kuja kumsaidia shughuli mbali mbali ikiwemo ya kupunguza gharama za nauli kwa dogo huyo kwenda shule.
Mama akiendelea na jukumu la kumuweka sawa mwanae katika swala zima la udereva wa Baiskeli.
sasa Zoezi limemalizika na Mama akijinyoosha kutokana na kuinama kwa muda mrefu wakati akimshikilia mwanae.daahh.... nakumbuka enzi zangu najifunza Baiskeli nilikuwa napenda sana kupitisha mguu mmoja kati ya bomba,ambapo hapo nilikuwa naweza kwenda umbali hata wa kilometa 100.kweli watu tumetoka mbali.



No comments:
Post a Comment