HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 10, 2012

ATCL yarejesha safari za Dar es Salaam kwenda Comoro

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATCL Mwanamvua Nguchu akisalimiana na maafisa usalama wa uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni mara baada ya ndege hiyo kuwasili nchini humo.
======  ======  =========
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) jana limerejesha safari ya kutoka  Jijinin Dar es Salaam  kuelekea Hahaya nchini Comoro ikiwa katika mpango wa kutekeleze mango wa miaka mitano wa maendeleo wa shirika hilo ambao unalenga kuongeza idadi ya ndege na pamoja na safari za shirika hilo. Shirika hilo lilifuta safari zake za Dar es Salaam – Hahaya mwaka 2008.

Akizungumza mara baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Prince Said Ibrahim mjini Hahaya, Comoro jana,  Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL, Mwanamvua Ngocho alisema kuwa shirika hilo la ndege la taifa litakuwa likifanya safari zake mara nne kwa wiki katika njia hiyo na kuahidi kuendelea kutoa huduma zilizo bora.

 “Leo hii tumezindua upya safari yetu ya Dar es Salaam – Hahaya (Comoro) ikiwa ni safari yetu ya kwanza ya kimataifa tangu tuliporejesha utoaji wa huduma  miezi miwili iliyopita. Tumeamua kuizindua upya safari hii ili kuitumia vilivyo ndege yetu ya Boeing 700-500 ambao ilikuwa haina kazi baada ya kumaliza safari ya Dar- es Salaam-Mwanza-Kilimanjaro asubuhi.

 “Tumeamua kuchagua njia hii kutokana na umuhimu wake kiuchumi nchini. Tunaimani kuwa jitihada zetu zitasaidia kuongeza mahusiano mazuri baina ya nchi hizi mbili na vile vile kutoa naafasi kwa abiria kutoka Comoro kusafiri sehemu mbalimbali kupitia Dar es Salaam,” alisema Bi. Mwanamvua.

Bi. Mwanamvua alisema kuwa kampuni yake bado inampango wa kujikita katika kuongeza safari za ndani na nje ya nchi akizitaja safari hizo kuwa pamoja na Dar es Salaam – Lusaka, Dar es Salaam – Johannesburg huku akisisitiza kuwa mipango hiyo itakamilika endapo Shirika hilo litapata ndege niyngine katika muda mufupi ujao.
 “Tayari tuko katika mazungumzo ya kupata ndege nyingine ambayo itatusaidia kujikita katika safari za kimataifa. Katika mpango huo tutashirikiana kibiashara na baadhi ya makampuni ya ndege ili kuweza kulifanikisha hili.

 “Tunawashukuru watanzania kwa uzalendo na imani wanayoionyesha kwetu tangu tuliporejesha utoaji wa huduma . Baada ya kutekeleze mpango wetu wa maendeleo kikamilifu,” aliongeza. Mwanamvua alisema kuna fursa nyingi za kibiashara ambazo zitajitokeza baada ya Shirika hilo kuanzisha safari za Comoro huku akiwataka Watanzania kuchangamkia fursa hizo ipasavyo.

“Bidhaa nyingi zitumikazo nchini Comoro zinatokea Tanzania. Wananchi wanatakiwa kuitumia fursa hii ipasavyo kutokana na ukweli kwamba ATCL itatoa huduma ya usafirishaji kwa bei nafuu. ,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad