
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 7 kwa Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha "Shujaa wa Safari Lager" kilichomalizika usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mahusiano TBL,Steven Killindo.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akimkabidhi Tuzo ya "Shujaa wa Safari Lager" Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Katikati anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Mil. 1 kwa Mercy Shayo ikiwa ni kama kifuta jasho kwa kuweza kufika katika hatua ya tatu bora.katikati ni Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mh. Makongoro Mahanga na kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mahusiano TBL,Steven Killindo akimkabidhi Bw. Leonard Mtepa mfano wa hundi ya shilingi Mil. 1 ikiwa ni kama kifuta jasho cha kuweza kufika hatua ya tatu bora.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akitangaza mshindi wa Tuzo za "Shujaa wa Safari Lager" usiku huu.huku Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja (katikati) na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah wakisikiliza.

Shujaa wa Safari Lager,Bw. Paul Luvinga akionyesha Tuzo yake huku akiwa ni mwenye furaha nyingi.

Mh. Mahanga akipeana mkono na Bw. Leonard Mtepa ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watatu waliofika katika hatua ya tatu bora ya Shujaa wa Safari Lager usiku huu.


Baadhi ya Wageni waalikwa.

Mie na Warembo,kulia ni Jamilah na Sylvia.

Warembo.

Majaji wajijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah.

Makamu Mwenyekiti wa UVCCM,Mh. Beno Malisa (kulia) akiwa na Mdau Victor Lebulu (shoto) pamoja na Mdau wa Kampuni ya Executive Solition.

Wanahabari wakifuatilia mchakato wa kupatikana Shujaa wa Safari Lager.

Wadau wa Kampuni ya Intergrated wakifuatilia shunghuli hiyoo.

Mjomba Band ikitumbuiza wimbo wao wa Shujaa wa Safari Lager katika hafla hiyoo.
No comments:
Post a Comment