Saturday, January 29, 2011

charles baba wa twanga pepeta afiwa na mama yake mzazi


Mwanamuziki Mahiri wa bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" Charles Gabriel (Charles Bab) pichani amefiwa na mama yake mzazi Asha Ramadhani Kilolege.

Msiba huo umetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi tarehe 29-01-2011 katika Hopsitali ya Mwananyamala baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria na Kisukari.

Mazishi yanataraji kufanyika katika Makaburi yaliyopo kwenye mashamba ya familia yaliyopo Chalinze kwa mwarabu.

Marehemu ameacha watoto 11.

Tunamuombea kwa Mungu aiweke roho Marehemu mahala pema peponi

-Amin

No comments:

Post a Comment