Monday, January 31, 2011

lakini kwa kuwa hakuna aliedhurika,basi ni poa tu na hakuna noma wala nini......

hivi ndivyo viendeshwavyo viombo vya moto katika maeneo mbali mbali jijini Dar,hii ni jioni ya leo katika baadhi ya mitaa ya kariakoo.

Sunday, January 30, 2011

WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini leo katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.

Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),

Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba
Mkurugenzi wa Vodafone Foundation wa Egypt, Noha Saad kushoto akisaini kitabu cha wageni katika hospitali ya CCBRT mara baada ya kutembelea hospitalini hapo na wakurugenzi wenzake Mwamvita Makamba,Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo wakiwa na lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa mdomo wa sungura na fistula kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya CCBRT walipotembelea hospitalini hapo kwa lengo la kujionea ni jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fetula na wa mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo,katikati Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Uingereza Andrew Dunnet,Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Tanzania Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa hospitali ya CCBRT Tom Vanneste akifafanua jambo kuhusu ugonjwa wa mdomo kisungura na fistula kwa maafisa wa Vodafone M pesa Afrika walipotembelea hospitalini hapo hawapo pichani kujionea jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.

kituo hiki ni kizuri sana kwa kweli na kinavutia hasa kwa jinsi kilivyotengenezwa na kupangiliwa namna ya kupaki mabasi hayo.
si mnaona jamani kinavyopendezaa........
kimbembe kinaanzia hapa sasa,hata sijui ni kwanini wameamua kuanzisha dampo mahala hapa.
hebu chekini takata zilivyojazana hapa,hivi ndio muendelezo wa matumizi ya kituo hiki au inakuwaje??maana mie nimeshindwa kuelewa kabisa.hebu wahusika fanyieni kazi swala hili maana hata haipendezi kwakweli.

Serikali ya Marekani ya Rais Barack Obama jana, Ijumaa, Januari 28, 2011, ilitangaza kuwa inatoa kiasi cha dola za Marekani milioni mbili (sawa na zaidi ya sh bilioni mbili) kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wa Mradi wa Uendelezaji Kilimo Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

Hatua hiyo ya Serikali ya Marekani ambayo kwa pamoja na Serikali za Tanzania na Vietnam inasaidia kusukuma utekelezaji wa mipango mipya ya kuboresha kilimo katika Tanzania na Vietnam, chini ya visheni mpya ya “A New Vision for Agriculture”, ni moja ya hatua nyingi zilizochukuliwa na Serikali hiyo kuunga mkono jitihada za Tanzania kufanikisha Mradi huo.

Mchango huo mkubwa wa Marekani ulitangazwa jana na Mtendaji Mkuu na Mtawala wa Mfuko wa Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa wa Marekani (USAID) Dkt. Rajiv Shah wakati alipoungana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuutangaza Mradi huo kwenye mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari mjini Davos, Uswisi.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari ambako Dr. Shah pamoja na viongozi wengine wakuu wa mashirika makuu ya kibiashara 17 duniani wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi huo waliunga na Rais Kikwete, kiongozi huyo wa USAID alitangaza:

“Tunakushukuru Rais Kikwete kwa kutushirikisha katika mkutano huu wa kwako na waandishi wa habari hasa wakati huo ambako bei za vyakula duniani zinaonyesha dalili za kuanza kupanda tena. Marekani inayo kila dhamira ya kuunga mkono Mradi huu ili uweze kufanikiwa na kufikia malengo yake,” alisema Dkt. Shah na kuongeza:

“Ili kuonyesha dhamira ya Serikali ya Marekani katika kuunga mkono Mradi huu, ninayo furaha ya kutangaza mchango wa nyongeza wa Marekani katika mfuko wa uwezeshaji wa Mradi huu wa kiasi cha dola za Marekani milioni mbili.”

Tanzania inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 50 kama mfuko wa kuanzisha SAGCOT ambayo uwekezaji wake unatarajiwa kufikia kiasi cha sola za Marekani bilioni 3.4 katika miaka 20 ijayo. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mkoa ongozi katika kilimo cha chakila ambayo ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma.

Mshiriki mwingine kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Hugh Grant ambaye ni Mwenyekiti, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mansanto ya Marekani inayojihusisha na kilimo duniani alisema kuwa mpango huo wa kilimo katika Tanzania na Vietnam utatumia mbegu za asili katika nchi hizo na siyo mbegu zilizotengenezwa kisayansi za GMO.

“Kwa sasa mipango yetu ni kutumia mbegu za jadi katika nchi hizo mbili – mbegu za asili, mbegu safi, mbegu zinazoweza kuhimili magonjwa na wadudu katika nchi hizi mbili. Hizi ndiyo mbegu zinazoweza kuwa za maana katika Mradi huu.“ Grant aliwaambia waandishi wa habari.

Kuhusu uwezekano wa makampuni 17 ya kimataifa yanayoshiriki katika kufanikisha Mradi huu kupanga bei za mazao yatakayozalishwa chini ya Mradi huu, Rais Kikwete aliwaambia waandishi wa habari:

“Kiasi kikubwa cha mazao kitakachozalishwa chini ya Mradi huu kitakuwa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata chakula cha kutosha. Kama kuna ziada, basi bei za mazao hayo ya ziada, zitaamuliwa na kiwango cha bei kwenye soko la kimataifa.”

Naye Paul Polman, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever katika Uingereza alisema kuwa mazao yatayozaliwa katika Tanzania chini ya Mradi huu yatakuwa na soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.

“Kuna mahitaji makubwa ya chakula duniani. Baadhi ya watu wanaishi kwa kutegemea kiasi kisichofikia dola moja ya Marekani kwa siku. Kuna watu wanatumia kiasi cha asilimia 70 ama 80 cha kipato chao kununua chakula. Lazima dunia izalishe chakula zaidi kwa sababu dunia isiyokuwa na chakula cha kutosha itakuwa ni dunia isiyokalika.”

Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari wa kimataifa, Rais Kikwete alikutana na kuwa na mazungumzo na Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Andrew ambaye ni mwakilishi maalum wa Uingereza kuhusu masuala ya biashara ya kimataifa na uwekezaji.

Katika mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumzia nafasi za Uingereza kuwekeza katika Tanzania na jinsi Tanzania inavyoweza kuwekeza katika uchumi wa Uingereza kama inataka na inao uwezo huo.

Baadaye jioni ya jana, Rais Kikwete alikutana na Waziri Mkuu wa Norway, Mheshimiwa Jens Stoltenberg na pia kukutana na Bwana na Bibi Bergman ambao wamekuwa wasaidia huduma za afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hasa Kitengo cha Tiba ya Meno.

Kabla ya kuondoka mjini Davos kwenda Addis Ababa, Ethiopia leo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika, Rais Kikwete alikuwa na mfululizo wa mikutano kwenye Hoteli ya Sheraton ya mjini Davos alipokuwa amefikia.

Rais Kikwete amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Accenture Development Partnership, Bwana Gib Bulloch kujadili jinsi gani teknolojia ya kisasa ya habari inavyoweza kutumika katika ufundishaji wa masomo katika shule za Tanzania.

Rais pia amekutana na kuzungumza na Bwana John Davies, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Intel anayeshughulikia na masoko na pia amekutana na Dkt. Nkosana Moyo, Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kuzungumzia jinsi gani benki hiyo inavyoweza kuchangia maendeleo ya SAGCOT.

Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Bwana Richard T Clark, Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Dawa ya Merck ambako mazungumzo yaliyohusu kuhusu maandalizi ya kupatikana kwa dawa ya kuwezesha chanjo ya kinga la kansa ya shingo ya kizazi dhidi ya akinamama wa Tanzania iliyopangwa kuanza mwaka ujao.

Saturday, January 29, 2011

Msanii Redsun kutoka nchini Kenya akikamua katika usiku wa Versity Nite ndani ya New Club Maisha.
Beka a.k.a Masuspender akifanya vitu vyake.
Vijana wa kazi toka T.H.T,Barnaba,Beka na Amini wakikamua vilivyo katika usiku wa Versity Nite ndani ya New Club Maisha,jijini Dar.
Belle 9 nae hakua nyuma katika makamuzi hayo ya ukweli kabisa ya Versity Nite.
Ukumbi ulifurika kwa uwingi wa wadau waliohudhuria usiku huo.

katika pita pita zangu za Mtaa kwa Mtaa,leo niliibukia mitaa ya Tandale Uzuri na kukutan na kisa hiki ambacho mwanadada huyo aliekaa chini alijikuta akitembezewa kichapo na jamaa mmoja hivi ambaye aliingia mitini.kisa cha kutembezewa kichapo dada huyu,inasemekana ni kwamba alikunywa bia za mshkaji huyo alieingia mitini na kukataa kuondoka nae.hapo ndipo jamaa alipatwa na hasira na kuanza kumuangushia kichapo hicho hadi wasamalia wema walipoanza kukusanyika na kumfanya msela huyo kuingia mitini.hiki ndicho kisa cha Uswahilini leo.
Wasamalia wakijaribu kumstiri kwa mavazi baada ya yale ya kwake kuchafuka vibaya na kuchanika pia.
Msaada ukiendelea.
kina mama waliokuwepo eneo la tukio wakijaribu kumuinua mwanadada huyo aliekuwa ametembezea kichapo mchana huu.


Mwanamuziki Mahiri wa bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" Charles Gabriel (Charles Bab) pichani amefiwa na mama yake mzazi Asha Ramadhani Kilolege.

Msiba huo umetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi tarehe 29-01-2011 katika Hopsitali ya Mwananyamala baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria na Kisukari.

Mazishi yanataraji kufanyika katika Makaburi yaliyopo kwenye mashamba ya familia yaliyopo Chalinze kwa mwarabu.

Marehemu ameacha watoto 11.

Tunamuombea kwa Mungu aiweke roho Marehemu mahala pema peponi

-Amin


The Government has reiterated its position on the planned tarmac highway around the Serengeti National Park to ease transport problems facing poor communities surrounding the Park, saying it will still go ahead and build the road.

However, contrary to what groups lobbying against the planned highway have been claming, the Government insists the highway will not be built through the Serengeti, which has been aclaimed internationally as the World Heritage Site.

The Government position was articulated yesterday (Thursday, January 27, 2011) by the President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete during his bilateral talks with the Managing Director of the World Bank, Ms. Ngozi Ikonjo-Iweala at the margins of the World Economic Forum (WEF), which both the President and Mrs.Ikonjo-Iweala are attending in Davos.

“Contrarary to what some people are saying, and to the rumours being circulated everywhere, my Government has never decided to build a tarmac road through the Serengeti,” President Kikwete told Ms Ikonjo-Iweala.

President Kikwete told the World Bank Managing Director that the Government plan seeks to severely reduce the length of the current road passing through the Serengenti National Park.

He said that currently a 220-kilometre unpaved road was running through the Serengeti and that the Government want to reduce it to only 54 kilometres that will pass through the National Park and those 54 kilometers will remain unpaved.

“Currently, 220 kilometres of road are passing through Serengeti National Park, right in the middle of the Park. And there is huge traffic crossing the park with large lorries and huge buses. We are unhappy with this situation. We want to reduce the length of road going through the Serengenti to only 54 kilometres passing mainly through the northern tip of the Park,” said President Kikwete.

He added: “This planned highway will meet three major objectives. One, is to reduce the flow of traffic passing the Park. Second, is to reduce the length of the road running through the Serengeti and third is to empower those poor communities living just outside the Serengeti to have a reliable road going through their area.”

“Some of the accusations against the Tanzania Government on this issue are quite absurd. People sit in Dar es Salaam and listen to all these people and institutions which are paid to say bad things about the Government, said the President and added:

“ Tanzania has the most impacable record in conservation in the world. About 20 per cent of our land has been under conservation since our independence in 1961. We are a leading nation in conservation in the world. How, then can we make decisions that would destroy the Serengeti? We would be the last people to destroy the Serengeti.”

President Kikwete has advised those who are interested in getting accurate facts about Government plans on the road supporting poor communities surrounding the Serengeti National Party to talk to the right people.

“We have a responsibility to our people. They need a road and we will deliver it to them while fully preserving our beloved Serengeti National Park,” said President Kikwete in relation to the long-running campaign against this road mainly by non-governmental organisations (NGO’s) and some conservation groups.

huu ni upendo wa dhati kabisa anaouonyesha kijana huyu ambaye ni mlemavu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.hapa alikuwa akimvisha mkufu aliokuwa amepewa na mmoja wa wapita njia katika barabara ya Morogoro Rodi mchana wa leo.