HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 15, 2026

Wachimbaji Wadogo Wapata Ustadi wa Kisasa Katika Kituo cha Mfano cha STAMICO KATENTE - GEITA

BUKOMBE - Juhudi za Serikali kuwainua wachimbaji wadogo nchini zinaendelea kuzaa matunda, huku zaidi ya wachimbaji 1,019 wakinufaika na mafunzo ya nadharia na vitendo katika kituo cha mfano cha Katente kilichopo wilayani Bukombe, Mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steve Kiruswa, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini. Dkt. Kiruswa alisisitiza kuwa wachimbaji wanaofika kwenye kituo hicho wamekuwa wakifanikiwa kuzalisha dhahabu safi kwa muda mfupi kutokana na teknolojia ya kisasa inayotumika.

"Wachimbaji wadogo wamekuwa wakileta marudio yao hapa na kuondoka na dhahabu safi kwa haraka. Hii inathibitisha umuhimu wa kuwawekea miundombinu mizuri na teknolojia rafiki," alisema Dkt. Kiruswa.
Akizungumza wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Subira Mgalu, aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo. Alitoa wito kwa STAMICO na Wizara ya Madini kuongeza na kupanua vituo vya mfano ili kuwafikia wachimbaji wengi zaidi kwa haraka.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Deusdedith Magala, aliwashukuru wajumbe wa Kamati kwa kuridhika na uwekezaji wa Shirika hilo unaolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa jamii.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad