Friday, July 18, 2025


Dar es Salaam, 18 Julai 2025

Mwandishi wa vitabu vya kuelimisha watoto, Bi. Riziki Mohamed Juma, amezindua rasmi kitabu chake kipya kiitwacho “Saburi” katika hafla iliyofanyika katika Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.

 Uzinduzi huu uliambatana na utambulisho wa vitabu vingine vya watoto, vikiwemo vya maandishi ya kawaida na vya nukta nundu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.

Vitabu hivi vimetolewa kwa ushirikiano kati ya Mtalimbo Books na Dhahabu Publishers, na vinapatikana katika maduka ya vitabu na maktaba za jamii nchini.

Saburi ni hadithi ya kuvutia inayowasilisha ujumbe kuhusu athari za utoro shuleni kwa njia rahisi na ya kufundisha. Ni kitabu kinachofaa kwa watoto, wazazi, walezi na walimu.


 

Na Mwandishi Wetu.

Mawaziri wa Mawasiliano kutoka Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Tanzania unaosimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), na mikongo ya baharini ya Mombasa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (ICTA).

Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidigitali wa Kenya, Injinia William Kabogo Gitau, pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania, Mhe. Jerry Silaa.

Mawaziri hao wamesisitiza kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria, ikilenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika, pamoja na kupunguza changamoto za kukatika kwa mtandao.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Gitau amesema: “Jambo la msingi ni ushirikiano wa dhati kati ya nchi zetu mbili. Ni muhimu kuhakikisha tunatunza miundombinu hii ya kimkakati ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababisha kukatika kwa umeme na mtandao. Pia tuendelee kuimarisha mahusiano yetu kwa manufaa ya pande zote.”

Kwa upande wake, Mhe. Jerry Silaa alisema kuwa ujenzi wa miundombinu ya pamoja ya mawasiliano kati ya nchi washirika ni wajibu wa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya kikanda.

“Kuna faida kubwa ya kuwa na maunganisho mengi ya mikongo ya mawasiliano. Hii husaidia kuwepo kwa mtandao wa uhakika, unaotegemewa hata wakati wa changamoto za kiufundi katika njia moja ya mawasiliano,” alisema Silaa.

Mkongo huo tayari umeanza kufanya kazi nchini Kenya, hatua inayowezesha huduma za intaneti na mawasiliano kusambaa kwa kasi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Uzinduzi huu unaashiria mafanikio makubwa katika juhudi za kuunganisha ukanda huu kidigitali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 



KILA mwaka Julai 18 dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa kutenga angalau dakika 67 kufanya huduma ya kijamii, kama njia ya kumuenzi shujaa huyo wa Afrika Kusini aliyejitolea maisha yake kupigania haki za binadamu, amani, usawa na utu wa mwanadamu.

Katika kuadhimisha siku hii muhimu mwaka huu 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Afrika Kusini waliungana kwa dakika 67 za huduma ya kijamii katika Makao ya Watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limewakutanisha watumishi wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa kidiplomasia, wadau wa maendeleo, na wanachama wa Jukwaa la Biashara kati ya Afrika Kusini na Tanzania.

Washiriki walijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo kusafisha mazingira, kupanda mimea ya bustani na kusaidia kazi za jikoni, kama ishara ya mshikamano na moyo wa kujitolea aliouacha Mandela.

Jukwaa la Biashara la Afrika Kusini na Tanzania pia walichangia vifaa muhimu kwa ajili ya makao ya watoto wenye mahitaji Maalumu, hatua iliyodhihirisha mshikamano wa sekta binafsi na taasisi za kimataifa katika kusaidia jamii.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,  Susan Namondo amesema;
“Leo tunamuenzi Madiba si kwa maneno bali kwa vitendo. Kila tendo la huduma—hata liwe dogo vipi, huchangia katika kujenga utu, heshima na matumaini. Ushirikiano wetu wa leo ni ushahidi wa nguvu ya umoja na mshikamano.”

Siku ya Nelson Mandela ni wito kwa kila mtu duniani kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wengine. Kauli mbiu ya Mandela “It is in your hands” inakumbusha kuwa kila mtu anao uwezo wa kuleta mabadiliko, hasa kwa wale walio katika mazingira magumu.

"Kwa pamoja, Umoja wa Mataifa Tanzania, Ubalozi wa Afrika Kusini, na wadau wengine wamesimama kwa moyo mmoja kuendeleza urithi wa Mandela kupitia huduma, mshikamano na matumaini." Amesema




Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP mkoani Njombe.

Kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Bilioni 4.360 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya madarasa, maabara, mabweni, Bwalo la chakula Jengo la Utawala na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Njombe ambayo imekamilika.

Hayo yamebainishwa tarehe 17 Julai 2025 na Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Njombe Mwl Nelasi Mulungu ambapo amesema pia Bilioni 1.6 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Amali ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya ya Ludewa.

Mwl Mulungu amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Bilioni 12.638 kwa ajili ya ujenzi wa shule 20 za kata katika mkoa huo wa Njombe.

Pia amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika mkoa wa Njombe ikiwemo ujenzi wa Mabweni, Nyumba za walimu, na Matundu ya vyoo.




Thursday, July 17, 2025

 


KUANZIA Julai 1 hadi Julai 30, 2025, Meridianbet imewapa wachezaji wake wa Win&Go dhamana ya kushiriki tena mchezo huo pendwa. Kwa mwezi mzima, ukipoteza Sh. 1,000 ama zaidi kwa siku, kesho Meridianbet itakurudishia 10% ya hasara yako kama Win&Go bonus, hadi kiwango cha juu cha Sh. 15,000 kwa kila siku.

Mfano halisi wa namna bonasi hii inavyokua ni kwamba unaingia mchezoni na ukiweka dau la Sh. 10,000 halafu mchezo usiwe upande wako basi kesho utapokea Sh. 1,000 kama asilimia 10% ya gawio la mchezo wa jana, hii inamaanisha unakua tayari kwa raundi ijayo bila hofu.

Bonasi hii ni injini ya nguvu inayovunja hofu ya hasara, yaani unacheza kwa malengo ya faida na kuingiza kipato, sio kwa woga wa kupoteza pesa yako na kukosa dau la kunzia kesho. Win&Go, mchezo wa tofauti uliotengenezwa na Expanse Studios, ukiwa na sifa kubwa ya kukupa matokeo kila baada ya dakika tano.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Uchezaji wake ni rahisi sana, unachagua namba 6 mpaka 10 kati ya 48, kisha mfumo unachezesha na ushindi hutokea pale namba zako ulizozichagua zinapotokea. Yaani ni mchezo wenye burudani na msisimko wa hali ya juu sana. Unacheza kwa lengo la kuingiza faida lakini pia ukiburudika.

Matokeo ya mchezo hayapo tu kwenye namba zako. Mfumo wa “gift positions” unaleta kasi mpya, pale namba yako inapotoka kwenye nafasi maalum (kama 12 au 23), utafurahi, utaonekana kama umecheza bure kwani dau lako linarejeshwa hata kama haukushinda. Zaidi ya hayo, kuna Golden Rounds, raundi maalum ambazo zinaongeza mara mbili au zaidi kiasi cha ushindi wako. Haya yote yanalengwa kuongeza msisimko na kuongeza mapenzi yako kwenye mchezo huu wa kasino mtandaoni.

Ofa hii inasaidia sana kwa wataalamu kama wewe, inakuwezesha kurudi mchezoni na mikakati mipya na kuanza tena ukiwa na msingi imara.

Masharti ni rahisi sana. Unacheza Win&Gobonasi inatolewa moja kwa moja hadi Sh. 15,000 na Meridianbet ina haki ya kubadili au kusitisha ofa ikiwa kuna utapeli, matumizi mabaya ya promo au matatizo ya kiufundi. Hakuna vikwazo vingi, si mchezo wa bahati ni mchezo wa akili tu.

Jisajili sasa na jukwaa pendwa kabisa, meridianbet ili uweze kushiriki Win&Go na bonasi hii iweze kukufikia pia, kwani hii bonasi ni fursa kwa kila mwana meridianbet.







MASHINDANO ya Gofu kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wa zamanı wa timu ya taifa ya wanawake ya gofu, marehemu Lina Nkya msimu wa nne yameanza kurindima rasmi leo katika Viwanja vya Lugalo Gofu jijini Dar es Saaalm.

Jumla ya wachezaji 150 wakiwemo 68 wa kulipwa na chipukizi na 82 wachezaji wasindikizaji wamesajiliwa kushiriki mashindano hayo ambayo yameanza leo Julai 17 na yatamalizikia Julai 20 mwaka huu katika viwanja hivyo.

Shindano hilo limeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa lengo la kumuenzi mchezaji huyo Lina ambaye alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2011 walipotwaa taji la Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi, mratibu wa mashindano hayo Ayne Magombe amesema mashindano hayo yameanza leo na yanatarajiwa kumalizika Julai 20, 2025 na kwamba yanafanyika kila mwaka kwa kujumuisha klabu za wachezajii wote wanaopenda kushiriki mchezo huo kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Magombe amesema wapenzi wote wa mchezo huo wa gofu hasa waliopo Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi kushirkki kwani ni moja ya fursa ya kuendelea kukuza na kuboresha ubora wao katika mchezo huo.

“Mashindano ya Lina Tour ni endelevu, kwa sasa tuna mashindano matano kwa mwaka, lakini tukipata sapoti kwa wadau wengine tunaweza kuwa na mashindano mengi zaidi ili kukuza huu mchezo,” amesema Magombe

Naye Mchezaji wa Gofu kutoka klabu ya Kilimanjaro, Racheal Mushi amesema amejipanga vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na anamatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa anaibuka mshindi.

Amesema Lina PG Tour nii mnzuri kwani yanawaleta pamoja wachezaji mbalimbali hivyo amewaomba waandaaji wa mashindano hayo kuendelea kuandaa michuano hiyo ambayo ina lengo la kukuza vipaji katika mchezo wa gofu nchini.

“Niwaombe waandaaji waendelea kutuandalia michuano hii mizuri kwa sasa Tanzania lakini pia niwatake vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki ili kuweza kukuza vipaji tulivyokuwa navyo,” amesema

Kwa upande wa baadhi ya wachezaji wa kulipwa wa gofu kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam na Lugalo wamesema wamejiandaa vizuri kushiriki michuano hiyo na wanaamini wataibuka washindi.


Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa shule mbili za kisasa za Amali Wilayani Kibondo Mkoani Tabora na Wilaya ya Mlele mkoani Katavi zinazogharimu Shilingi Bilioni 3.2

Vilevile serikali imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 8.8 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule ya wasichana Rukwa iliyopo Wilayani Sumbawanga na Shule ya wasichana Katavi iliyopo Wilayani Nsimbo ambazo zote kwa pamoja zimeanza kutumika ili kuimarisha sekta ya elimu katika mikoa hiyo sambamba na nchi kwa ujumla wake.

Shule hizo zimejengwa kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) ikiwa ni eneo muhimu la utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kuhusu kuboresha sekta ya elimu nchini.

Miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya shule za wasichana Katavi na Rukwa ni pamoja na maabara za (Kemia, Fizikia, Baiolojia na Jografia), vyumba vya madarasa na ofisi, Vyoo, mabweni, nyumba za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo la TEHAMA, Mashimo ya maji taka pamoja na fensi.

Kwa upande wa Ujenzi wa shule mpya za Amali katika Wilaya ya Mlele mkoani Rukwa unahusisha ujenzi wa Madarasa na ofisi, Maktaba, Jengo la Utawala, Maabara za Kemia na Baiolojia, Jengo la TEHAMA, Mabweni 4, Bwalo la chakula, Karakana 2 za ufundi, Nyumba ya mwalimu, na Matundu ya vyoo.






16 Julai 2025 – Mwananyamala Hospital Dar es Salaam, Tanzania

Miss World @suchaaata Miss Africa @hasset_dereje na Mustafa @mustafahassanali walitembelea wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na Doris Mollel Foundation.

Wameguswa na kazi kubwa inayofanywa kuwahudumia watoto njiti na wamepongeza juhudi zinazofanyika na kuahidi kuchangia vifaa tiba na kusaidia hospitali nyingine zaidi kwenye maeneo yasiyofikiwa.





Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira amewakumbusha watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo kushirikiana na Wanahabari ili wananchi waweze kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi.

Wito huo ameutoa leo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo yaliyofanyika kwa siku tatu katika Kituo cha Tabora yaliyojumuisha watendaji kutoa Mikoa wa Tabora na Kigoma.

"Katika utekelezaji wa majukumu yenu, mtapaswa kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari ili kuwajulisha wananchi na wadau wa Uchaguzi mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi" alisema Mhe.Rwebangira.

Aidha Mhe.Rwebangira amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanatunza rasilimali vifaa vya Uchaguzi watavyovipokea kwaajili ya Uchaguzi sambamba na kuhakikisha wanafuata Sheria, kanuni na miongozo kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili wakatimizie jukumu la usimamizi wa Uchaguzi kwa weledi.

Mafunzo haya ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 yamekamilika leo tarehe 17 Julai, 2025.