- MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 26, 2023

 

Na.Khadija Seif, Michuziblog

KAMPUNI ya Big Solution watarajia kufanya kongamano maalum la kuwaunganisha pamoja wanaohusika na fani ya kupiga picha mnato na video mapema Juni 6, 2023 katika hoteli ya Mbezi Garden iliyopo Makonde, Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari leo 26, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Big Solutions, Rajab Mchatta amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja na kujadili changamoto zilizopo katika tasnia yao.

Mchatta ameongeza pia kongamano hilo litawakutanisha wapiga picha na wakufunzi ambao watatoa elimu ya masuala ya maadili, fursa za biashara na matumizi ya teknolojia.

Moja wa wapiga picha nguli nchini ambaye ni Mdhamini wa kongamano hilo Mkurugenzi wa DTP Hanif Abdulrasul amesema amevutiwa sana na wazo hilo na kusema kuwa litasaidia wapiga picha kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo elimu ya kuwekeza katika bima ya vifaa vya uzalishaji picha.

Naye Haika Lawele, Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel, ambao ni wadhamini wa ukumbi amesema wametoa eneo hilo kuanzia asubuhi hadi jioni ili kufanikisha tukio hilo la kuwakutanisha wapiga picha na kupata elimu ya maadili ya picha ili kuongeza ubora katika kazi zao.

Kongamano hilo limeandaliwa na kampuni ya Big Solutions Limited kwa kushirikiana na kampuni ya Desktop Publishing (DTP), Mbezi Garden Hotel, Jackie Events na Michuzi Media huku wakiomba wito kwa makampuni kujitokeza kuweza kudhamini tukio hilo.
Mkurugenzi wa DTP, Hanif Abdulrasul akizungumza na Wanahabari Leo Mei 26,2023 ambapo amesema ujio wa kongamano maalum la kuwaunganisha pamoja wanaohusika na fani ya kupiga picha mnato na video linalotarajiwa kufanyika mapema Juni 6, 2023 katika hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Big Solutions, Rajab Mchatta akizungumza na Wanahabari Leo Mei 26,2023 na kusisitiza watu wa fani ya upigaji picha za mnato na video kuhudhuria kongamano la siku 1 kwa ajili ya kuwaweka pamoja watu wa fani hiyo na kutoa mafunzo na elimu juu ya teknolojia mpya na kupanua sekta hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad