MENEJA TANROADS DODOMA: MRADI WA BARABARA YA MZUNGUKO KUKUZA UCHUMI WA MKOA WA DODOMA NA TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 18, 2023

MENEJA TANROADS DODOMA: MRADI WA BARABARA YA MZUNGUKO KUKUZA UCHUMI WA MKOA WA DODOMA NA TANZANIA

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
 
Mradi ujenzi wa varabara ya lami ya njia nne ya mzunguko (Outer Ring Road) ndani ya jiji la Dodoma itakayokuwa na urefu wa kilometa 112.3 unatajwa kuwa na manufaa makubwa ikiwemo katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Dodoma na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Faida nyingine za utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dodoma ambapo magari makubwa ambayo yanakwenda nje ya Dodoma hayatapita mjini yatapita katika barabara hiyo huku ajira zaidi ya elfu mmoja zikizalishwa kupitia mradi huo.

Hayo yamesemwa Aprili 18, 2023 na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Leonard Chimagu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa mbele ya waandisha wa habari ambapo amesema mradi huo umegawanywa mara mbili na kutekeleza na wakandarasi wawili tofauti.

Mhandisi Chimagu ameendelea kwa kusema kuwa, kipande cha kwanza kitahusisha ujenzi wa kuanzia Nala-Veyula-Barabara ya Arusha-Mtumba-Ihumwa (bandari kavu) ikiwa na urefu wa kilometa 52.3 ambapo mkandarasi kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na kugharamu kiasi cha shilingi bilioni 100.84

"Ujenzi wa kipande cha pili cha barabara hiyo unaanzia Ihumwa (bandari kavu)-Matumbulu-Nala itakayokuwa na urefu wa kilometa 60 ambao mkandarasi wa kampuni ya AVIC International na kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 120.86" alisema Mhandisi Chimagu

Akiongelea miradi mingine katika mradi huo, ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zinazoendelea wilayani Mpwapwa zikiwa na urefu wa zaidi ya kilometa 50 na pia barabara kwa kiwango cha lami ya urefu wa kilometa 23 itajengwa kuelekea hospitali ya Mvumi.

Vilevile Mhandisi Chimagu amesema, ndani ya Mkoa wa Dodoma kuna mradi unasanifiwa ambao utahusisha ujenzi wa barabara za lami katikati ya jiji la Dodoma zikiwa na urefu wa 43.

Kwa upande wake Mhandisi wa miradi kutoka TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Colman Gaston amesema, kwa upande wa kipande cha pili cha barabara hiyo kutoka Ihumwa (bandari kavu) hadi Nala utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 18.4 huku ukiwa na faida lukuki kwa jamii.

"Hadi kufika sasa mkandarasi amekamilisha kazi kwa asilimia 18.4, mradi huu umekuja na miradi mingine ya kijamii ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya ambapo vitajengwa vituo vya afya vinne vikiwa na gari ya kubebea wagonjwa (ambulance) pamoja na uchimbaji wa visima vinne" alisema Mhandisi Colman

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wahandisi washauri katika mradi huo kutoka kampuni za Inter consultant and Pace na CTC Crown Tech Mhandisi Issa Mjema na Mhandisi Lusekelo Kijalo matawalia wamesema, watasimamia kazi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kabla ya muda uliopangwa ambao ni mwezi Machi, mwaka 2025.

Mikataba miwili ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa Barabara ya lami ya njia nne ya Mzunguko (Outer Ring Road) ndani ya Jiji la Dodoma itakayokuwa na urefu wa kilometa 112.3 na kuwa barabara ndefu za aina hiyo kuliko zote katika Nchi za Afrika Mashariki na Kati na kutatua changamoto ya msongamano wa magari jijini Dodoma ilisaniwa Julai 10, 2023 baina ya Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa niaba ya Serikali na wakandarasi wawili Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na AVIC INTL Project Engineering Company walioshinda zabuni ambao watajenga barabara hiyo kwa kipindi cha miezi 36. Mkandarasi Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), atajenga kilometa 52.3 kuanzia Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port na mkandarsi AVIC INTL Project Engineering Company atajenga kilometa 60 itakayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu hadi Nala.
Wafanyakazi  wa kampuni zinazotengeneza Barabara hiyo  wakiwa katika majukumu yao ya kazi.
Mmoja wa Wakandarasi  wanaosimamia mradi huo kutoka kampuni ya Avic akizungumza na Waandishi wa habari.
Picha ya Juu ya moja ya Makaravati makubwa yanayojengwa katika mradi wa Barabara ya Mzunguko Mkoani  Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad)  Mhandisi Leonard  Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad