MSAJILI WA HAZINA AANIKA MIPANGO, MIKAKATI YAO KWA TAASISI ZA UMMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 19, 2023

MSAJILI WA HAZINA AANIKA MIPANGO, MIKAKATI YAO KWA TAASISI ZA UMMA

 Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MSAJILI wa Hazina Nehemiah Mchechu ameeleza sababu za kukutana na taasisi mbalimbali za umma ikiwemo kuweka mikakati ya kufanya mageuzi makubwa katika utendaji wa taasisi za umma pamoja na kukumbushana majukumu yao na kufanya mabadiliko ya kiutendaji ili kuleta tija.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 19,2023 ,Mchechu ameanza kueleza kazi ya Msajili wa Hazina ni kusimamia taasisi zote za umma karibia 300 lakini pia kusimamia uwekezaji wa Serikali,kuishauri Serikali na kusimamia taasisi zilizobinafsishwa.

Amesema Sasa huo ndio wajibu wao mkubwa kuona kwamba kunakuwa na manufaa makubwa kwenye uwekezaji uliofanywa na Serikali na kwamba kwa ujumla mpaka sasa kuna kiasi cha Sh.trilioni 70 kwenye mashirika mbalimbali ya biashara na siyo ya biashara akitolea mfano kuanzia mabenki, mashirika ya ujenzi, hospitali,vyuo vikuu vyote,

"Katika hizi taasisi lazima zitengeneze faida, lazima zijitegemee zisiwe mzigo kwa Serikali.Leo tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana wajibu ,wajue majukumu ya TR, wajue mabadiliko yanayofanyika katika ofisi ya Msajili wa Hazina lakini wajue matarajio na nia ya Serikali kuona mabadiliko na ufanisi katika taasisi zote za umma ,kila unapona SU au Wakala

"Kwa hayo baada ya kikao hiki cha taasisi tutakuwa na utendaji kazi wa karibu zaidi,kuwa na ufanisi, na maana yake mapato ya Serikali yanakwenda kuongezeka kwa maana ya changio kwenye gawio, pamoja na hiyo lakini taasisi hizi zinapofanya vizuri kulingana na huduma zake zinazidi kutamalaki. Kwa hiyo ndio ilikuwa lengo kubwa na kesho tutakuwa tunamalizia na taasisi nyingine kama 170,"amesema Mchechu.

Kuhusu changamoto,amesema zipo nyingi lakini ukweli uchangiaji wa taasisi umepungua lakini kiwango kimeongezeka, hivyo lengo lao ni kuona kunakuwa na uchangiaji mkubwa na kiwango kikubwa ndicho ambacho wamekuwa tunakitimiza sasa hivi .

"Tunakwenda vizuri lakini tunatakiwa kwenda zaidi ya hapa tunavyofanya sasa, tunafanyia kazi agizo la kuleta mabadiliko na tuko kwenye hatua nzuri na tutakuwa tunafanya mawasilisho.

Akizungumzia mashirika yaliyokuwa yakitoa gawio kwa Serikali na sasa hayatoi, amesema wanajaribu kuangalia changamoto ni kwanini sasa hivi walikuwa wanatoa na sasa hawatoi gawio.Inawezekana changamoto ni mitaji au matatizo tofauti ,huenda ikawa mitaji, wengine hawana uongozi imara kama uongozi sio imara tunawakumbusha.

"Na kama hawakumbushiki tutafanya mabadiliko , kwa hiyo kauli ya Rais anataka kuona mabadiliko , ni jambo ambalo linaenda kutekelezeka ,tuko makini na yeye yuko makini ,kama mtu hajajipanga vizuri kwenye eneo analosimamia maana yake kuna Watanzania wengine watakaoweza kuendesha vizuri mahali pale."

Mchechu ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba mageuzi ambayo wanakwenda kuyafanya ni pamoja na kupata viongozi, watakavyopima kazi zao, utekelezaji wao pamoja na vigezo vinavyotumika kwa sekta na sekta huku akifafanua wamewapanga kwenye makundi ya sekta na wao wenyewe wanajifanyia mageuzi ili waweze kufiti.
Msajili wa Hazina,Nehemiah Mchechu akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara unaendelea leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dares Salaam.

(PICHA NA EMMAMUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)

Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara wakimsikiliza Msajili wa Hazina,Nehemiah Mchechu (hayupo pichani)

(PICHA NA EMMANUEL MASAKA WA MICHUZI TV)

Mkutano ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad