DC KWIMBA AANZA KUGAWA VYANDARUA VYENYE VIATILIFU KUDHIBITI MALARIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 20, 2023

DC KWIMBA AANZA KUGAWA VYANDARUA VYENYE VIATILIFU KUDHIBITI MALARIA

MKUU wa Wilaya ya Kwimba Ng'wilabuzu Ludigija amezindua ameanza kampeni ya kugawa vyandarua vyenye Viatilifu katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba kwa lengo la kukabiliana na Malaria sambamba na kuzindua mpango wa kudhibiti Malaria kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja katika chanjo ya kwanza ya Surua, Rubella(miezi 9), wajawazito katika hudhurio la kwanza.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog, leo Aprili 20,2023 , Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Kudigija amesema makundi mengine ambayo yapo kwenye kampeni hiyo ni wazee wenye umri miaka 60 na kuendelea, watoto wenye umri chini ya miaka 5 wanapoenda kutibiwa malaria, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wanapoenda kupata huduma za VVU.

Amesema vyandarua hivyo vitatolewa kwa mzunguko wa miaka miwili kwa makundi hayo na vina nembo ya Bohari ya Dawa (MSD) na kwamba huo ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita katika mpango wake wa kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030 na kuongeza umiliki wa vyandarua kwa jamii angalau asilimia 80.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad