MISSANGA AUNGANA NA WANA SEPUKA ,MWARU NA IRISYA KWA KUTOA IFTAR, WAMUOMBEA DUA RAIS Dkt. SAMIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 15, 2023

MISSANGA AUNGANA NA WANA SEPUKA ,MWARU NA IRISYA KWA KUTOA IFTAR, WAMUOMBEA DUA RAIS Dkt. SAMIA

 

Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kutoa Futari kwenye Jamii  Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ndugu Ahmed Missanga  ameungana na Waumini Mbalimbali katika Msikiti Mkuu wa Sepuka Wilayani Ikungi katika  kutoa Iftari na Dua Maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi  mbalimbali wa Mkoa Singida.

 Kabla ya Dua hiyo comrade Missanga pamoja na taasisi ya Faraja trust fund pamoja na sheikh wa Mkoa wa Singida  walitembelea Gereza Kuu la Singida na kuwapelekea Wafungwa sadaka ya Futari na mahitaji mbalimbali. 

Mjumbe  wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ndugu Ahmed Missanga anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini  na Mkoa wa Singida Ramadhani njema.

Kwa upande wake Imamu wa Msikiti wa Sepuka Sheikh Jumanne Mohamedi Mughenyi  pamoja na Imamu wa Msikiti wa Mwaru sheikh Omari Mgisa  na Imamu wa Msikiti wa Irisia sheikh Jumanne Kungu wamemshukuru sana Kiongozi huyo kwa kutoa iftar katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan na mawaidha aliyoyatoa kuhusu kuwalinda Vijana dhidi ya vitendo vya mmomonyoko wa Maadili  na kuwataka  Wazazi kuendelea kukemea vitendo vinavyohatarisha ukiukwaji wa Maadili ya Mwafrika.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad