Benki ya NBC yaandaa futari kwa ajili ya wateja wake Zanzibar, Spika Zubeir aguswa na mchango wake kiuchumi na kijamii - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 31, 2023

Benki ya NBC yaandaa futari kwa ajili ya wateja wake Zanzibar, Spika Zubeir aguswa na mchango wake kiuchumi na kijamii

 

Zanzibar: Machi 31, 2023:  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar huku Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar , Zubeir Ali Maulid akiionyesha kuridhishwa na mchango wa benki hiyo katika usatwi wa uchumi wa visiwa hivyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika hotel ya Madnat Al  Bahr, Zanzibar Spika Zubeir alionyesha kuridhishwa na namna benki ya NBC inavyoshirikiana na Baraza hilo pamoja na Serikali katika kuleta maendeleo visiwani Zanzibar kupitia huduma zake mbalimbali kama La riba pamoja na mchango wake kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.

“Pamoja na yote hayo zaidi niwapongeze NBC kwa kuonesha umuhimu wa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata kwa namna mbalimbali  ikiwemo kwa njia hii ya kufutarisha, uimarishaji wa huduma za afya ( mobile Clinics), kuchangia afya ya uzazi salama n.k Pamoja na  huduma nyengine mbali mbali kwa jamii tunashukuru,’’ alisema.

Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi, Mkurugenzi wa mikopo wa benki hiyo Bw Salehe Mohamed alieleza kuwa  hatua hiyo ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa miaka 9 sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

“Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo.” Alisema Mohamed.

Zaidi alibainisha kuwa benki hiyo ina huduma maalum inayojikita katika kutoa huduma kwa wateja wake wa imani ya Kiislam, yaani Islamic Banking inayopatikana kwenye matawi yote ya benki hiyo ikiendeshwa katika misingi ya dini hiyo ikiwa na huduma mbalimbali ikiwemo akaunti ya La Riba.

Aidha Mohamed aliwaomba wale ambao hawajajiunga na benki hiyo kufungua akaunti zao ili waweze kufurahia huduma bora na za kipekee zinazotolewa katika matawi yote ya NBC nchini.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla  ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyoSpika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (wa pili kushoto) akiwaongoza wageni waalikwa pamoja na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC kuomba dua ya chakula  kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyoMkurugenzi wa mikopo wa Benki ya NBC Bw Salehe Mohamed (Kulia) akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (kushoto) zawadi maalum wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyoSpika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC akiwemo Mkurugenzi wa mikopo wa benki hiyo Bw Salehe Mohamed (katikati) na Mkurugenzi wa wateja Binafsi wa Benki hiyo Bw Elibariki Masuke (Kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyoSpika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (wa pili kulia) sambamba na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC akiwemo Mkurugenzi wa mikopo wa benki hiyo Bw Salehe Mohamed (wa tatu kulia)  wakiwaongoza wageni wengine waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Bw  Ramadhani Lesso akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na serikali, viongozi wa dini, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo visiwani Zanzibar wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad