CHONGOLO AAGIZA TAMISEMI KUKAMILISHA HARAKA ZAHANATI AMBAYO UJENZI WAKE UMEKWAMA KWA ZAIDI YA MIAKA 10 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 2, 2023

CHONGOLO AAGIZA TAMISEMI KUKAMILISHA HARAKA ZAHANATI AMBAYO UJENZI WAKE UMEKWAMA KWA ZAIDI YA MIAKA 10

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameiagizaa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupeleka fedha haraka kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kinambeu iliyopo Iramba mkoani Singida.

Ujenzi wa Zahanati hiyo umekwama kwa zaidi ya miaka 10 hali ambayo imeendelea kusababisha changamoto na adha kubwa Kwa wananchi katika kupata huduma za afya na hivyo kulazimika kutembea umbali mrefu.

Katibu Mkuu Chongolo ametoa maelekezo hayo kwa TAMISEMI baada ya kupokea taatifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo ulianza mwaka 2011 lakini hadi sasa haijakamilika.

Chongolo alifika kwenye Zahanati hiyo Kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi na majengo yaliyopo lakini kutokana na hali aliyoona amelazimika kutoa maelezo hayo kwa TAMISEMI .

"Naiagiza TAMISEMI na Halmashuri ya Iramba kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo ili wananchi waondokane na adha ya kukosa huduma za afya."

Zahanati hiyo ujenzi wake hadi sasa umegharimu Sh.Milioni 185.9 ambapo Mhisani kutoka Japan alitoa Sh. Milioni 158.8, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Sh.Milioni 20.04 na jamii kutoa nguvu kazi zenye gharama ya Sh.Milioni 7.06 na mkandarasi aliishia kukamilisha kazi ya ujenzi wa kuta na kupaua Desemba mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad