KAMPUNI TAIFA GAS YAELEZA ILIVYOJIPANGA KUENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2023

KAMPUNI TAIFA GAS YAELEZA ILIVYOJIPANGA KUENDELEA KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI

 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Taifa Gesi nchini imeeleza hatua kwa hatua mipango yake kwa kushirikiana na wadau wengine wa gesi katika kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati ya gesi ikiwemo ya kuja na mitungu ya kilo tatu ambazo kila mwananchi anaweza kumudu kununua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la Shirikisho la Kampuni za Gesi Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla, Mkurugenzi wa Taifa Gas Hamis Ramadhan amesema kwenye kongamano hilo watapata nafasi ya kujadiliana masuala mbalimbali ili kukuza sekta hiyo.

Aidha amesema kupitia maonesho yanayoendelea pia wataangalia teknolojia zilizopo zinazoweza kutumiwa na kampuni na wananchi wote kuendeleza matumizi ya gesi endelevu ya gesi.

“Katika kongamano hili kutakuwa na mijadala ambayo tutabadilishana mawazo namna tunavyoweza kukuza matumizi ya gesi nchini ili kuachana na yale madhara ya mkaa na kuni ambayo wote tunayafahamu ya kimazingira na kiafya

“Kwa hiyo tunawageni mbalimbali kutoka nje ya nchi, tunawatalaamu kutoka sekta ya gesi , tuna viongozi wa kiserikali, wananchi , waandishi wa habari na kikao hicho kinawapa nafasi ya kupata vitu vizuri ambavyo tutatumia kuongeza matumizi ya gesi Tanzania,”amesema.

Kuhusu mikakati ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akihamasisha, amesema kuna vikao vingi vinafanyika vya kiserikali ,wakuu wa mikoa mbalimbali na wabunge wamekuwa wakikutana na wanagawa mitungi ya gesi pamoja na kuhamasisha kutumia matumizi ya gesi.

“Sasa kila eneo wanafanya kwa nafasi yake , sisi hapa tumejikusanya wadau wa gesi tukitaka kuleta teknoloji itakayosaidia ukuzaji wa matumizi ya gesi pamoja na kubadilisha mawazo. Kwa hiyo waliko hapa ni kwa namna ambavyo tunaendelea na ule uhamasishaji uliofanywa na Serikali.

“Wote tuko hapa kwenye njia moja ya kukuza matumizi ya gesi Tanzania, na ni utekelezaji ambao unaendelea kutokana na kuhamasishana kama sekta binafsi.Rai yangu niwaombe watanzania wa kawaida washiriki kwenye vikao hivi ni vizuri.

“Wafanyabiashara walioko mitaani waje ili wapate ujuzi na waone sehemu ya maonesho , kwasababu kuna vifaa vya matumizi ya gesi, kuna vifaa vya ufundi ambavyo vinaoneshwa na wakishiriki kwenye mjadala itakuwa vizuri. Kwa hiyo tunahamasisha wafike wapate elimu ambayo wataipata bure kwani kampuni za gesi na wadhamini wameshaigharamia,”amesema.

Kuhusu ni hatua gani zinaendelea ili kuhamasisha wananchi wengi kutumia gesi , Mkurugenzi huyo wa Taifa Gas amesema ili watu wengi watumie gesi ni vema wakawa wanapeleka kiwango kidogo kama vile wanavyonunua mkaa kila siku kwani itakuwa rahisi.

“Teknolojia huwa ina vipindi vyake, wakati mwingine unaweza ushindwe kwenda lakini mitungi ya kilo tatu sasa hivi ipo , kampuni kama ya Taifa Gas ambayo mimi ni Mkurugenzi wake tuna mitungi ya kilo tatu na kimsingi inapendwa na inatumiwa na watu wengi

“Mitungi ya kilo mbili bado tunaifanyia utafiti na tuna uhakika wasambazaji wenzetu wa gesi wanaliangalia hilo suala , tutaenda mpaka pale kiwango cha chini ya kujaza kitaruhusiwa kitendaji , kwa hiyo mitungi ya kilo tatu ipo na bei yake kujaza ni Sh.13000,”amesema Ramadhan.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha LPG Tanzania Amos Mwansumbue ameeleza kwenye kikao hicho kuna mijadala inayoendelea na washiriki watakuwa na fursa kupita kwenye maabanda yaliyoko kwenye Maonesho hayo ambapo mtu atapita kuangalia, hivyo amewaomba wanaojihusisha na biashara za gesi kufika .

"Tumeona huko mtaani kuna vifaa vibovu vinatumika kwa mfano Valvo, Regulatter, ukitumia kifaa ambacho sio salama kwenye gesi kinaweza kuleta matatizo ,kwa hiyo ni vizuri vile vifaa vinunuliwe kutoka kwa watengenezaji au wauzaji ambao kitalaam na Kimataifa wameidhinishwa kufanya kufanya hiyo kazi kwasababu ukinunua vifaa vilivyotengenezwa huko mtaani ambavyo sio salama unaweza kuhatarisha usalama wa maisha na tunaweza kuleta matatizo katika biashara ya gesi

"Kwa hiyo malengo ya mkutano huu ni kuelimisha lakini pia kuwafahamisha watu wote wanaohusika na gesi waweze kujifunza bidhaa mbalimbali zinazohusiana na gesi,"amesema Mwansumbue.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba kupitia Chama Cha LPG Tanzania watahakikisha wale wote wanaofanya kazi katika sekta ya gesi wamepitishwa na wanakidhi viwango vya kufanya zile kazi, kwa mfano ukimuita fundi achomolee bomba kwenye ghala linalohifadhi gesi huyo fundi je anaoutalaam wa kutosha wa kuchelea hilo bomba.

" Kwa hiyo tunataka fundi kama hiyo apitishwe kwenye utalaamu wa namna ya kutengeneza hivyo vifaa vya gesi au miundombinu ya gesi aweze kufanya kazi kwa usalama zaidi.Kingine ambacho ni cha muhimu sana hiki Chama kinataka kutengeneza nidhamu kwenye soko ,nidhamu ya wauzaji.

"Tunajua wateja wetu wengi mara nyingine wananunua gesi unakuta haina uzito unaotakiwa,uko kidogo kwasababu kuna wauzaji ambao wako mtaani wanachukua mtungi wa kampuni ambazo zipo anayenda anafaulisha kwenye mitungi mfano wa kilo 38 kwasababu inakuwa na bei ndogo anachukua anakwenda kubadilisha kwenye mitungi midogo, hivyo kufanya ujaza kuwa mdogo, hana kipimo na mteja hawezi kujua maana hakuna anayasema nipimie.Hivyo tunataka kusimamia nidhamu."

Mkurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gasi Hamis Ramadhan akizingumza na waandishi wa habari kwenye Kongamano la Kimataifa la Wadau wa Gesi Afrika Mashariki linaloendelea jijini Dar es Salaam sambamba na Maonesho ya Teknolojia mbalimbali zinazotumika kutengeneza vifaa vya gesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania LPG Association, Amos Mwansumbue (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonesho ya gesi ya kupikia (LPG EXPO Afrika Mashariki 2023) yaliyo anza leo tarehe 15 hadi 16 mwezi huu jijini Dar es salaam.  
Mkurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas Hamis Ramadhan (kulia) akiwa makini kufuatilia majadiliano mbalimbali wakati wa kikao cha Kongamano la mkutano wa Kimataifa uliohusisha Kampuni za gesi kutokana maeneo mbalimbali duniani.Sehemu ya washiriki walifuatilia mkutano huo unaendelea jijiini Dar es Salaam.
Majadiliano yakiendelea wakati wa Kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad