
Na Mwandishi Wetu
Mtanzania Deogratius Mosha, ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha uvumbuzi kwenye teknalojia kwa wavumbuzi wenye umri chini ya miaka arobaini kutoka barani Afrika, maarufu kama Forty under 40 Awards.
Mashindano hayo ambayo huandandaliwa na kampuni ya Xodus Communications ya nchini Ghana na kuwashindanisha viongozi wa biashara na wavumbuzi mbali mbali kutoka Afrika, zimefanyika Cape Town, nchini Afrika ya Kusini.
Lengo la mashindano hayo ni kuwatambua viongozi na wavumbuzi wenye umri chini ya Miaka 40 wanaochipukia katika nyanja mbalimbali barani Afrika. Kwa mwaka huu, mashindano hayo yameshirikisha zaidi ya washiriki 126 kutoka nchi mbali mbali za barani Afrika.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Bw. Deogratius alisema mashindano haya yamekuwa yakisaidia kuleta chachu kwa viongozi na wavumbuzi wa Kiafrika wanaochipukia.
“Mashindano haya hutoa hamasa kwa wavumbuzi wa Kiafrika na kuwafanya kuendelea kufanya juhudi zaidi katika nyanja mbalimbali, hasa katika masuala ya teknolojia. Kwangu mimi ushindi huu ni ujumbe wa kuleta hamasa zaidi kwa vijana haswa Wakitanzania kujiamini na kushiriki kushindana kwenye masoko ya kimataifa. Kufanya hivyo kutatuwezesha kukuza uchumi na kupanua wigo wa soko letu la ajira,” alisema
Deogratius Mosha alishiriki katika kipengele ya Teknolojia na Ubunifu, akiwa kama Mkurugenzi mwanzilishi wa Kampuni ya Mainstream Media Limited ya hapa nchini ambayo imebuni mifumo mbalimbali ikiwamo mfumo wa kuwezesha taasisi za kifedha kusajili wateja kidijitali, Pamoja na uvumbuzi wa mifumo kwa wanafunzi wa vyuo kujisomea kidijitali kupitia simu zao maarufu kama SmartUni App.
Watanzania wengine waliobuka vinara kwenye nyanja tofauti ni Bi. Naike Moshi Wa CV People , Bi. Catherine Kakolo Mongella - Earth Guardians na Dr. Jesca Mhoja Nkwabi - Kom Group Of Companies
Deogratius ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuja na programu mbalimbali za kuwasaidia na kuwezesha vijana kujikita katika masomo ya sayansi hasa kupitia kwenye vituo atamizi vilivyopo nchi nzima. Pia ametoa Rai kwa vijana kuweja juhudi katika mambo yanayoleta tija kwa Maisha yao binafsi na taifa kwa ujumla ili kuweza kukuza uchumi wanchi

MWISHO…..
No comments:
Post a Comment