Mstahiki Meya wa Ubungo azitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB uboreshaji wa elimu nchini - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 12, 2023

Mstahiki Meya wa Ubungo azitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB uboreshaji wa elimu nchini

 Na mwandishi wetu 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo,  Jaffary  Nyaigesha amezitaka  taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya DCB katika juhudi zake za  uboreshaji wa elimu nchini.

Mstahiki meya aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati akipokea msaada wa madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kiluvya, iliyo katika Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam yaliyotolewa na DCB kupitia kampeni yake ya ‘Elimu Mpango Mzima na Mama Samia’.

“Kwa kufanya hivi, Benki ya DCB inaunga mkono juhudi za Rais wetu Mpendwa, Mheshiwa Dk. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watu wake maendeleo katika uboreshaji wa elimu nchini”, alisema mstahiki meya.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bwana Isidori Msaki akizungumza mahali hapo alisema,madawati hayo ni sehemu ya madawati 150 yeye thamani ya shs 37,500,000 wanayoyatoa katika Manispaa tano za jiji la Dar es Salaam ikizingatiwa kuwa wao ndio wanahisa  waanzilishi wakati benki ikianzishwa miaka 20 iliyopita.

“Tunajivunia ushirikiano wenye tija na Manispaa hizi kwani kwa kipindi cha miaka 20 kwa mtaji wa shs bilioni 1.7 tuliokuwa nao mwaka 2002, benki imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na imeweza kutoa gawio la jumla ya shs bilioni  11.5 kati ya hizo Manispaa zikipokea gawio la shs bilioni 4.55”, alisema Bwana Msaki.

Mkurugenzi huyo alisema, mafanikio haya yanawezekana chini ya uongozi mahiri wa Bodi ya benki hiyo inaoongozwa na mwanamama shupavu Bi. Zawadia Nanyaro.

“Ni matumaini ya DCB kuwa msaada  utazidi kuimarisha mahusiano kwa manufaa ya pande zote mbili, DCB kama mtoa huduma za kibenki na mdau wa maendeleo na kwa manispaa  yako kama wadau wetu muhimu”, alisema. 


.Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary Nyaigesha ( wa tatu kushoto ) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya  msaada Madawati 30 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki ( katikati ) kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni muendelezo  wa kampeni ya benki hiyo inayoendelea ya elimu iitwayo ‘Elimu Mpango Mzima na Mama Samia’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya  msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary  Nyaigesha akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya  msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam Jana.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominick akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya  msaada wa madawati 30 na Benki ya Biashara ya DCB kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam jana.

 Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffary Nyaigesha ( wa tatu kushoto ) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki baada ya kupokea msaada madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Shule ya Msingi Kiluvya, Leah Sanga akizungumzia maendeleo ya shule yake  wakati wa hafla ya makabidhiano ya  msaada wa madawati 30 na Benki ya Biashara ya DCB kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Alisema ufaulu wa darasa la Saba unaongezeka mwaka hadi mwaka. 2020 asilimia 91; 2021 asilimia 96.2; na 2022 asilimia 96.5

 Diwani Kata ya Kibamba, Peter Ikamba akitoa neno la shukrani baada ya  kukabidhiwa msaada wa madawati 30 na Benki ya Biashara ya DCB kwa ajili ya shule ya msingi Kiluvya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’  shuleni hapo, Kiluvya, Ubungo jijini Dar es Salaam jana





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad