MAKAMU WA RAIS KATIKA MJADALA WA UWEKEZAJI KWA WATU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 6, 2023

MAKAMU WA RAIS KATIKA MJADALA WA UWEKEZAJI KWA WATU

 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango
ameshiriki katika mjadala uliobeba ajenda ya Uwekezaji kwa Watu Wote
Pasipo Ubaguzi ulioshirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki
Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea za Kipato cha
Chini unaofanyika Doha Nchini Qatar.

Akichangia katika mjadala huo, Makamu wa Rais amesema katika kuwekeza
kwa watu Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo
kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na
sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuboresha
miundombinu ya shule pamoja na ujenzi wa shule za wanawake maalum kwa
masomo ya sayansi kila mkoa wa Tanzania.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba ili kuendana na wakati wa sasa,
Tanzania inafanya mabadiliko ya mitaala ya kufundishia pamoja na kujikita
katika elimu ya tehama kwa kutoa vifaa vya kidijitali kwa walimu ili waweze
kufanikisha lengo hilo. 

Pia amesema ili kuhakikisha elimu inakua jumuishi bila
ubaguzi, Tanzania imefanikiwa katika kuwarudisha masomoni wanafunzi
walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo za
kupata ujauzito.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa
kuendelea kuunga mkono mataifa yanayoendelea kutokana na uwepo wa
changamoto katika uwekezaji kwa watu ikiwemo kukosekana fedha za
kutosha katika kuboresha na kuongeza vyuo vya ufundi, upungufu wa vifaa
vya kujifunzia hususani kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na
ufinyu wa miundombinu ya kujifunzia kutokana na ongezeko la watu.

Makamu wa Rais yupo nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa
Nchi Zinazoendelea za Kipato cha Chini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango. akizungumza katika mjadala uliobeba ajenda ya Uwekezaji kwa Watu Wote Pasipo Ubaguzi ulioshirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea za Kipato cha Chini unaofanyika Doha Nchini Qatar.(Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mbarouk N. Mbarouk nje ya Ukumbi wa Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea za Kipato cha Chini unaofanyika Doha Nchini Qatar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad