MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA DAR ES SALAAM ATETA NA KAMISHNA WA SKAUTI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2023

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA DAR ES SALAAM ATETA NA KAMISHNA WA SKAUTI

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Dar ea Salaam Khadija Ally Said amepata fursa ya kufanya mazugumzo na Kamishna wa Skauti Mkoa huo Amina Maulid na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu ushirikiano.

Mengine ni kujua mchango na utayari wa Chama cha skauti katika utoaji wa mafunzo,  elimu na malezi ya watoto na vijana kwa ujumla  na namna ambayo jumuiya ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Februari 20,2023 na Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam ,katika mazungumzo hayo wamejadiliana kwa kina kuhusu  kushirikiana na Chama cha Skauti Dar es Salaam kama wadau na kutoa mchango wa pamoja kwenye kulinda maadili ya watoto na vijana kwa ujumla.

Aidha kuelimisha kuhusu mmong'onyoko wa maadili na athari zake unaojitokeza kwenye jamii yetu kwa kasi kubwa sasa hivi na kwamba 

Jumuiya ya wazazi Dar es salaam imeazimia kushirikiana na Skauti Dar es salaam kuwa na Klabu  za Skauti katika kata zote 102 za Mkoa huo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad