AFISA MKUU UENDESHAJI WA CPS ZANZIBAR AZUNGUMZIA KUHUSU SERA ZA NYUMBA NA UANZISHWAJI WA VIWANDA KWENYE KONGAMANO LA EUBG TANZANIA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 27, 2023

AFISA MKUU UENDESHAJI WA CPS ZANZIBAR AZUNGUMZIA KUHUSU SERA ZA NYUMBA NA UANZISHWAJI WA VIWANDA KWENYE KONGAMANO LA EUBG TANZANIA.

 

Bi. Katrin Dietzold, Afisa Mkuu wa Uendeshaji CPS Zanzibar ametoa maoni yake kuhusu fursa na uwezeshaji wa sera bora ya makazi na uanzishwaji wa viwanda kwenye mjadala wa kongamano la EUBG Tanzania, uliofanyika February 23, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Wakati wa jopo la mjadala huo, Bi. Katrin Dietzold alibainisha fursa za sera bora ya nyumba katika kufungua fursa kubwa ya sekta ya majengo Zanzibar na kuwapatia makazi bora wakazi wa zanzibar wanaoongezeka kwa kasi. Alisisitiza kwamba kwa kuwa na sera na mifumo sahihi, sekta ya majengo Zanzibar inaweza kuleta manufaa katika uchumi na jamii kwa kiasi kikubwa.


Bi. Katrin pia alielezea uzoefu wake kwenye maeneo ya uanzilishi wa sekta ya majengo huko Zanzibar, akisisitiza kuwa serikali na soko zinahitaji watendaji wenye ubunifu ili kukabiliana na changamoto zinazoletwa na teknolojia mpya ya ujenzi. Aliwahimiza wadau wengine katika sekta hiyo kuja Zanzibar kwa lengo la wazi lakini lenye upeo wa kubadilika kadri siku zinavyoenda. Uvumilivu, ustahimilivu na utu vinahitajika ili kufikia mafanikio.


Alieleza faida za kufanya kazi Zanzibar, na kubainisha kuwa serikali inafikika na mazingira ya kufanyia kazi yanadhibitika kulinganisha na sehemu kubwa ya Tanzania. Bi Katrin aliwahimiza waendelezaji wengine kuangalia Zanzibar kama ardhi yenye rutuba kwa ukuaji na upanuzi wa biashara, ambayo pia ina fursa zisizoisha kwa wale walioko tayari kukabiliana na changamoto.


Ushiriki wa CPS Zanzibar katika kongamano la EUBG Tanzania unaonyesha dhamira ya kampuni hiyo katika kukuza maendeleo endelevu katika sekta ya majengo nchini Tanzania. Mtazamio wa kampuni wa ubunifu wa maendeleo, unaodhihirishwa na mradi wake wa Fumba Town (Fumba Town project), umeweka kiwango kipya cha uendelevu wa sekta hiyo na athari chanya jamii yake.


Mji wa Fumba, mradi ulioanzishwa na CPS, ndio mradi wa maendeleo ya majengo unaouza kwa kasi zaidi Tanzania ambao tayari umeuza zaidi ya nyumba 1000 na unawapa wamiliki wa nyumba wenye utambuzi duniani kote nafasi ya kuishi, kufanya kazi na kujiendeleza katika mazingira salama, endelevu, ya kimataifa, ya kitamaduni na vizazi mbalimbali. Mji huo mashuhuri tayari ukusanya wanunuzi kutoka zaidi ya nchi 50, na hivyo kuonyesha mkazo katika mvuto wake mkubwa wa kimataifa.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa CPS, Katrin Dietzold (wapili kulia) akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye kongamano la EU Tanzania business forum wakati wa mada ya "Wekeza Zanzibar " ili kutoa fursa na uwezeshaji uliopo kupitia sera za majengo. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango - Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Ahmed H.Saadat, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Shariff Ali Shariff na Meneja wa kisiwa cha Chumbe coral park, Benjamin Taylor

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad