SERIKALI YATOA BILIONI 60 KUANZA UJENZI BARABARA YA LAMI LIKUYUFUSI-MKENDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 18, 2023

SERIKALI YATOA BILIONI 60 KUANZA UJENZI BARABARA YA LAMI LIKUYUFUSI-MKENDA

 

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 60 kuanza ujenzi barabara ya lami kilometa 60 kutoka Likuyufusi  Kwenda Mkenda Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Barabara hiyo ni ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji yenye urefu wa kilometa 124 ambayo ina Kwenda hadi katika daraja la Mkenda Mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi  Ephatar Mlavi amesema serikali kwa kuanzia inatekeleza mradi huo kwa kilometa 60  kuanzia  Likuyufusi Manispaa ya Songea hadi Mkayukayu Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

“Mradi huu utahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, sehemu ya Likuyufusi – Mkayukayu yenye urefu wa kilometa 60’’,alisema Mhandisi Mlavi.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad