RAIS MSTAAFU AWAMU YA SITA AFUNGUA TAMASHA LA BIASHARA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 5, 2023

RAIS MSTAAFU AWAMU YA SITA AFUNGUA TAMASHA LA BIASHARA

 

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 

Rais Mstaafu wa Awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume amewataka 

wafanya biashara kutoa risiti za electronik na wanunuzi  kudai risiti  ili kwenda na mabadiliko ya tekenolojia.

Dk. Karume ametoa wito  huo ameutoa katika Uwanja wa Maisara  wakati  akifungua   Tamasha la tisa la biashara ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kutimiza miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema risiti ni kitu muhimu katika biashara kwani inasaidia kuhifadhi upotevu wa fedha pamoja  kumrahisishia mfanyabiashara  kuweka mahesabu ya bishara  zake.

Aidha amefahamisha kuwa kuongezeka kwa matamasha kama hayo kunaimarisha fursa  ya wafanya biashara jambo ambalo linaimarisha uchumi wa Zanzibar.

Aidha Rais Mstaafu wa awamu ya sita amewaasa wafanyabiashara kuacha kufanya udanganyifu  kwa kupunguza vipimo au kuzidisha kwa lengo la kujipatia kipato jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya  nchi na dini.

Hata hivyo ameishauri Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda kufanya tathmini ya matatizo yaliyojitokeza katika tamasha hilo ili kuyafanya matamsha   mengine kuwa bora zaidi .

Nae Waziri wa Wizara hiyo  Omar Said Shaaban amesema kuwa kufanyika kwa tamasha hilo ni moja ya utekelezaji wa Serikali katika kuhamasisha uchumi wa biashara ili kuwa na mvuto wa kukuza mazingira ya kibiashara.

Aidha amefahamisha kuwa Serikali imeanzisha Tamashahilo kwa lengo la kuwafanya  biashara kuimarika zaidi kibiashara   na kujiongezea  kipato chao na taifa .

Ameeleza kuwa Serekali inaendelea  kuhakikisha kuwa inakuza mazingira ya biashara kwa kutafuta eneo la kudumu Nyamanzi ili wafanya biashara waweze kuimarisha biashara zao zaidi.

Hata hivyo Waziri huyo amezishukuru Taasisi za Serekali na Wafadhili mbalimbali ambao wameshirikiana na kwa pamoja kwa kutoa michango yao kuhakikisha Tamasha hilo linafanyika.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ali Khamis amesema kuwa kufanyika kwa Tamasha la biashara ni kuwasaidia wafanyabaishara ili kubadilishana uzoefu wa kutengeneza bidhaa bora zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa tamasha hilo limegharimu zaidi ya Shilingi 277 milioni ambazo zinatokana na michango ya wafadhili.

 Katibu Mkuu  huyo ameeleza kuwa tamasha hilo  linapata hadhi  kila mwaka kutokana na kukuwa kwake na kupata wageni kutoka maeneo mbali mbali .

Tamasha la biashara limewashkisha wafanya biashara mbalimbali wakiwemo kutoka  ndani na nje ya nchi ambapo kauli mbiu ya mwka huu USHIRIKISHWAJI WA JINSIA KWA MAENDELEO YA BIASHARA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad