SONGWE WAZINDUA WIKI YA SHERIA KWA MAANDAMANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 22, 2023

SONGWE WAZINDUA WIKI YA SHERIA KWA MAANDAMANO

 

Mkuu wa Wilaya ya Songwe,Mhe. Simon Simalenga amewaongoza Wananchi wa Wilaya ya Songwe kufanya maandamano ikiwa ni sememu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani humo leo Januari 22,2023 Makao Makuu ya Wilaya hiyo Kata ya Mkwajuni ambapo aliwataka Wananchi kutumia fursa hiyo kuuliza maswali ambayo yatalenga kutatua migogoro mbalimbali kama vile kwenye sekta ya Ardhi, Madini na Masuala ya Ndoa.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye tukio hilo kubwa na muhimu lililoandaliwa na timu ya Hakimu Mkaazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Songwe Mheshimiwa Augustin Lugome ni pamoja Mheshimiwa Philipo Mulugo (MB), Chesko Mbilinyi (Kaimu DAS), CPA Cecilia Kavishe (Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Songwe), Mahakimu, Mawakili, Watumishi wa Mahakama, Warumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Maweni, Mkwajuni na Sume na Wananchi wa Wilaya hiyo.

Katika kuhakikisha Wananchi wa Wilaya hiyo wanapata Elimu kuhusu masuala ya Sheria mbalimbali Muhimili wa Mahakama umepanga kufanya ziara kwenye vijiji 43 vya Wilaya ya Songwe vinavyounda Kata 18 ili kutoa Elimu kwa wananchi ambao walikuwa wanatembea kilomita 155 kwenda Wilayani Mbozi kupata huduma ya Kimahakama. Kwasasa Wilaya ya Songwe imeshapata Jengo lake la Mahakama ya Wilaya ambalo limeshaanza kutoa huduma husika kwa Wananchi.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad