JIMBO KATOLIKI LA MBULU LIMETOA DARAJA YA USHEMASI KWA MAFRATERI SITA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 7, 2023

JIMBO KATOLIKI LA MBULU LIMETOA DARAJA YA USHEMASI KWA MAFRATERI SITA

 

Na John Walter-Manyara

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema wametakiwa kuiombea miito mitakatifu ndani ya familia ili injili ya kristo, iwafikie wale wote ambao hawamtambui kristo.

Hayo yamo katika homilia takatifu, iliyotolewa na askofu wa jimbo Katoliki la mbulu Mhashamu Askofu Anton Lagweni wakati wa adhimisho la sadaka ya misa takatifu ya kutoa daraja ya ushemasi iliyofanyika katika kanisa la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni Parokia ya Sanu Jimbo Katoliki la Mbulu Januari 5, 2023.

Askofu Lagweni amesema kuwa shemasi anapokea paji la roho mtakatifu kwa ajili ya kupeleka neno la mungu kwa watu,na hivyo anapaswa kujitoa sadaka kwa ajili ya watu wa Mungu.

Akitoa salamu za pongezi, Mbunge wa jimbo la Mbulu Mjini  Zakaria Paul Issay amewapongeza mashemasi hao kwa kuitikia sauti ya Mungu huku akitoa wito wa kuendelea kuwaombea ili waweze kutimiza wito huo wa ukuhani walioitiwa.

Mashemasi waliopokea daraja hiyo ni shemasi Paulo John Pissa kutoka Parokia Ndogo Ya Bargishi Uwa Mbulu, Frateri Anton Baloho kutoka Parokia ya Geklum Lambo Karatu, Frate Paskali Bombo kutoka parokia ya Kateshi Hanang, Shemasi Joakimu  John Baran wa parokia ya Karatu,Shemasi John Masawe wa Parokia Ya Gitting, Shemasi Faustine Joseph wa Parokia ya Kiru.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad