POLISI WATOA RAI KWA WAZAZI NA WALEZI KUHUSU MALEZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 4, 2023

POLISI WATOA RAI KWA WAZAZI NA WALEZI KUHUSU MALEZI

 

Jeshi la Polisi nchini limetoa rai kwa wazazi na walezi kuhusu suala la kuimarisha
malezi ya familia hususani katika eneo la ukuaji wa watoto ili kuwaepusha
kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu pamoja na kuwaepusha kufanyiwa vitendo
vya ukatili.

Kauli hiyo imetolewa na Mrakibu wa Polisi SP Dkt. Ezekiel Kyogo kutoka Kamisheni
ya Polisi Jamii Dawati la Ushirikishwaji wa Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma
wakati walipotembelea kituo cha kulelela watoto wenye uhitaji mbalimbali
kiitwacho Chigongwe Family ambapo jamii imetakiwa kutowatelekeza watu
wenye uhitaji na badala yake kuendelea kuwasaidia.

Naye mmoja wa watoto wanaopatiwa malezi kwenye kituo hicho Paul Charles
amesema licha ya kutoka kwenye mazingira magumu lakini kwa sasa jamii
imejitokeza kuwasaidia kwa kuwapatia hifadhi na mahitaji mengine ya msingi.

Naye Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Manase Dotto kutoka Dawati la Usalama
Wetu Kwanza amesema kuwa, Jeshi la Polisi linaendelea kuwalinda watoto hivyo
waendelea kutoa ushirikiano sambamba na kuripoti vitendo vyovyote vya ukatili
watakavyofanyiwa ama kukutana navyo.
 No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad