SERIKALI YAKUSANYA MAONI USAFIRI MAJINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 6, 2022

SERIKALI YAKUSANYA MAONI USAFIRI MAJINI

 

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) imetoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri majini nchini kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni kwa usafiri wa huo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha siku moja kilichowakutanisha wamiliki hao wa Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dar es salaam Mkurugenzi Msaidizi-Utawala Sekta ya Uchukuzi Bw. Hamidu Mbegu amesema maoni ya wadau ni ya muhimu kwa mustakabali wa utoaji huduma bora na zenye viwango.

‘Maoni yenu ni ya muhimu sana kwa maboresho ya huduma zinazotolewa kupitia usafiri huu, ni imani yangu kuwa kwa siku hii mtapata fursa ya kuchakata kanuni zitakazowasilishwa, kuainisha changamoto zilizopo na kuja na maoni chanya yatakayoboresha ‘ amesema Mbegu.

Mkurugenzi Mbegu amesema pamoja na maoni hayo maeneo muhimu ya kushauri ipasavyo ni pamoja na kanuni zinazohusu Usalama wa usafiri kwa njia ya Maji, usajili meli, upakiaji na upakuaji wa Mizigo kwenye Meli, kanuni ya kudhibiti Meli kugongana baharini.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Sheria kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Judith Kakongwe amesema Serikali inafuta taratibu zote zinazptplewa na Shirika linalosimamia Usafiri wa Majini Duniani (IMO) kabla ya kutekeleza vipengele vilivyo kwenye mikataba ya kimataifa hivyo hiyo ni fursa muhimu kwa wadau hao kutoa maoni ili kuboresha kanuni hizo kulingana na mazingira yalioyopo.

Naye Mdau wa kikao hicho Captain King Chiragi amesema utekelezaji wa miongozo mbalimbali inayosimamia usafiri wa majini ina vipengele muhimu katika kuzingatia mazingira halisi tuliyopo hivyo kama wadau wako tayari wakati wote kutoa maoni kwa maslahi mapana ya uendeshaji wa usafiri huo.

Uwepo wa Mkutano huo wa wadau ni utekelezaji wa kisheria wa mikutano inayotakiwa kufanywa kwa kuwahusisha wadau kujadili na kuboresha sheria na kanuni za usafiri huo.Mkurugenzi Msaidizi-Utawala (Sekta y Uchukuzi) Hamidu Mbegu akifafanua jambo kwa wamiliki wa meli (hawapo pichani) wakati alipofungua kikao cha siku moja kilichowakutanisha wadau hao na Serikali kujadili kuhusu kanuni za usafiri wa majini, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

PICHA NA WUU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad