Mhe. Mchengerwa Atoa Siku 5 Kwa Watendaji kukamilisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 18, 2022

Mhe. Mchengerwa Atoa Siku 5 Kwa Watendaji kukamilisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa

 

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa ameiagiza  Idara ya Sanaa na Bodi ya Filamu kuhakikisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa unaanza kutoa mikopo kwa Wasanii ifikapo jumatano ya Desemba 21, 2022.

Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo usiku wa kuamkia  Desemba 18, 2022 jijini Arusha katika Usiku wa Tuzo za Filamu mwaka 2022, ambapo amepongeza Wasanii Kwa kuendelea kufanya filamu bora.

" Sekta ya Filamu inakua, na inaendelea kutoa ajira  Kwa vijana wengi pamoja na kuchangia katika Pato la Taifa, hivyo sisi kama Serikali tutaendelea kuweka nguvu katika Sekta hiyo" amesema Mhe. Mchengerwa.

Amesisitiza Watendaji wa Wizara kumaliza michakato iliyopo katika utekelezaji wa majukumu kwa wadau wa Sekta za Wizara yake, huku akiwaasa kuweka mazingira rahisi kwa wadau hao kutekeleza majukumu yao.

Katika tukio hilo Mhe. Mchengerwa alipokea Tuzo Maalum kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kukuza Sekta ya Filamu na Kuanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini.

Vilevile ametoa Tuzo Maalumu kwa Wasanii waliofanya vizuri na kutoa mchango katika kukua kwa Sekta ya Filamu. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad