MWENYEKITI CCM BUKOBA MJINI AVUNJA UKIMYA SAUTI INAYOZUNGUKA MTANDAONI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 4, 2022

MWENYEKITI CCM BUKOBA MJINI AVUNJA UKIMYA SAUTI INAYOZUNGUKA MTANDAONI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Joas Muganyizi Zachwa ameamua kuvunja ukimya baada ya kuwepo kwa clip ya sauti ambayo ni ya kutengeneza inayomhusu yeye akihusishwa kukutana na madiwani na Katibu wake wa zamani wa Chama.

Akizungumza kuhusu sauti hiyo Zachwa amesema ameona  clip ya audio( sauti) ikihusihwa na yeye akiwatukana madiwani na katibu wake wa zamani wa Chama ambapo amefafanua kwamba Clip hiyo ni ya kutengenezwa na ameanza kuchukua hatua za kisheria na kutaarifu vyombo vinavyohusika kushughulikia. 

"Najua hii inafanyika kutokana na mimi kusimamia maelekezo ya Ilani ya CCM na misingi ya Chama chetu ya kushughulikia kero za wananchi hasa wafanyabiashara.

"Nataka niwahidi wanaCCM wa Wilaya ya Bukoba Mjini, CCM na Serikali yake itabaki kuwa salama na hatutasita kuwasemea wananchi kwani ndio maelekezo ya Ilani na viongozi wakuu wa Chama. Mungu ibariki CCM, Mungu ibariki Tanzania."


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad