Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akutana Wadau mbali mbali wa Sekta ya Sheria - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 14, 2022

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akutana Wadau mbali mbali wa Sekta ya Sheria

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wasaidizi wa Sheria pamoja na Wadau mbali mbali wa Sekta ya Sheria wakati akifungua Jukwaa la Mwaka la watoaji wa msaada wa kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) Kampasi ya Maruhubi.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza katika Ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la watoaji Msaada wa Kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) Kampasi ya Maruhubi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF Bi Lulu Ngwanakilala akitoa Maelezo kuhusiana na jitihada mbali mbali wanazochukua katika kuwasaidia watoaji msaada wa kisheria wakati wa Ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la watoaji wa msaada wa kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) Kampasi ya Maruhubi.
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said akisoma maazimio ya Jukwaa ilipita la watoaji msaada wa kisheria na namna yalivyofanikiwa katika hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la watoaji wa msaada wa kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) Kampasi ya MaruhuWatoaji Msaada wa kisheria na wadau mbali mbali wa Sheria wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua Jukwaa la Mwaka la watoaji wa msaada wa kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Maruhubi.


Makamo wa Pili wa Rais Zanbar alipongeza shirika la LSF kwa utoaji msaada wa kisheria kwa wananchi wanyonge

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar,Hemed Suleiman Abdullah amelipongeza Shirika la Shirika la Legal Services Facility (LSF),kwa kuendelea na harakati mbali mbali za kuweza kuisaidia jamii ya Kizanzibari na Tanzania kwa ujumla katika mambo mbali mbali ya uatoaji msaada wa Kisheria na haki unapatikana hasa kwawananchi walio wanyonge.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumanne Tarehe 13 Disemba 2022 wakati akifungua kongamano la jukwaa la Pili la Mwaka la kujadili upatikanaji wa haki na namna ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria Zanzibar lililoandaliwa na Wizara ya ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na utawala bora visiwani humo kwa kushirikiana shirika la LSF.

Abdullah amesema,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana mchango unaotolewa na shirika hilo katika uimarishaji wa upatikanaji haki Zanzibar kwa wananchi wasio na uwezo na wenye

mahitaji maalum.

“Nawapongeza kwa kuendelea kushirikana nasi katika maadhimisho ya Wiki ya msaada wa Kisheria ambapo kwa mwaka huu 2022 maadhimisho yalienda vizuri,”amesema Abdullah

Pia amesema,Shirika hilo kwa kushirikiana na Afisi ya Rais-Katiba,Sheria,Utumishina Utawala Bora limeweza kufanikisha Jukwaa hili kwa lengo la kuweza

kujadili na kubadilishana uwezo kuhusiana na Watoaji msaada wakisheria. Pia,ameseama Serikali ya Awamu ya Nane kupitia Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi imejidhatiti vya kutosha katika kuhakikisha wananchi wake wanapata haki na wananchi wanafata Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Aidha,Mheshimiwa Abdullah amewataka watoaji Msaada wa Kisheria wa Sheria kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa kuzingatia maadili ili zilete tija na maendeleo yaliokusudiwa.

Hata hivyo ,Abdullah amewataka wasadizi hao kushirikiana na Serikali kutokomeza masuala ya ukatili na unyanyasaji.

“Naamini mnafahamu kwamba kwa sasa masuala ya udhalilishaji yamekuwa makubwa katika nchi yetu pamoja na uwepo wa migogoro ya ardhi na usajili wa matukio ya kijamii hususani vyeti vya kuzaliwa muendelee kuwa mstari wa mbele kuelimisha wananchi kuongana na serikali kutokomeza vitendo hivi “amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa LSF,Lulu Ng’wanakilala,amesema kongamano hilo ni matokeao ya kazi ya Shirika hilo chini ya Ufadhili wa DANIDA,katika kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya masaada wa Kisheria.

“Ni wazi kuwa LSF kupitia ufadhili wa DANIDA imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki katika muongo mmoja uliopita ndani ya Tanzania bara na Zanzibar,”amesema Lulu.

Pia,Lulu ameiomba Serikali ya Zanzibar ifanye marakebisho zidi ya sheria ya msaada wa kisheria ya 2018,ili iweke mazingira bora ya jinsi ya upatikanaji rasilimali za kuendesha huduma hizo ikiwemo kuweka mfuko wa msaada wa kisheria.

“Ni ukweli usiopingika kuwa ufadhili wa wadau wa maendeleo katika sekta hii unazidi kupungua siku hadi siku, na hivyo tunapaswa kwaharaka kuangalia jinsi

ya kubeba jukumu bila kuathiri ubora na upatikanaji wa huduma bora kwa jamii kabla matumaini ya wanufaika wetu hayajafifia,”amesema Lulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad